logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ibraah ajuta kumtukana Rayvanny kipindi cha ugomvi wake na Harmonize

Ibraah alisema kwamba aliwaho kuomba kolabo na Rayvanny lakini akaambiwa aanze na Macvoice kwanza.

image
na Davis Ojiambo

Burudani08 April 2024 - 09:51

Muhtasari


  • • Kambi ya Rayvanny akiwemo msanii wake Macvoice walishusha maneno huku Harmonize na msanii wake Ibraah wakijibu.
  •  
    • Lakini miaka miwili baadae, Rayvanny na Harmonize walikutana na kuyamalzia huku Macvoice na Ibraah wakibaki na tope kwenye nyuso zao.
Rayvanny na Ibraah

Msanii wa Konde Gang, Ibraah ameonekana kujuta kumtolea uvivu Rayvanny kwa maneno makali kipindi alipokuwa kwenye ugomvi mzito na bosi wake, Harmonize.

Akizungumza kwenye mahoajinao na kituo kimoja cha habari wikendi iliyopita, Ibraah alisema kwamba hakujua kwamba Harmonize na Rayvanny watakuja kupatana huku mbeleni na tukio la yeye kutunga wimbo akimtukana lilimkosesha kolabo.

Msanii huyo wa lebo ya Harmonize alifichua kwamba kipindi Fulani aliomba meneja wa Rayvanny kufanya kolabo na yeye lakini akajibiwa kwamba aanze kwanza na msanii wa Rayvanny, Macvoice.

“Mimi nishawahi kumuambia meneja bwana nisaidie kuongea na mzee [Rayvanny] basi ili tupate kufanya kolabo. Kwa sababu hawa ndio wameweza, unajua wao wamefanya vingi, kwa hiyo tu tuwadhihirishie watu kwamba tuko vizuri, lakini akanirudia akasema bwana tumesikia umesema unataka kolabo lakini anza na Macvoice kwanza,” Ibraah alisema.

Kwa sauti ya kujuta, Ibraah aliwaomba wasanii na mashabiki wake ambao huenda watausikiliza huo wimbo alioutunga kumtupia maneno Rayvanny na kusema kwamba wasichukulie kwa maanani sana.

“Mimi niwaambie wasanii wenzangu wa Tanzania kwamba haijalishi lakini mtakapokutana na vesi sijui nimemtukana kwenye wimbo, aah mashabiki zangu….” Alisema kabla ya mahojiano kukatika.

Itakumbukwa kipindi Rayvanny na Harmonize wamevimbiana mwaka 2021 kisa penzi la Kajaka kwa Harmonize ba bintiye Paula kwa Rayvanny, kulitokea vita kubwa ya maneno kutoka kwa kambi zote mbili.

Kambi ya Rayvanny akiwemo msanii wake Macvoice walishusha maneno huku Harmonize na msanii wake Ibraah wakijibu.

Lakini miaka miwili baadae, Rayvanny na Harmonize walikutana na kuyamalzia huku Macvoice na Ibraah wakibaki na tope kwenye nyuso zao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved