Akothee ameonyesha furaha yake baada ya mashabiki wake kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii kumsherehekea kwa njia maalum siku yake ya kuzaliwa.
Mjasiriamali huyo wa wakfu wa Akothee alipeleka kwenye mitandao ya kijamii kwenye kurasa zake na kufhihirisha furaha kutokana na jinsi mamia ya mashabiki wake walimsherehekea si tu kwa maneno matamu bali pia kwa zawadi kdhaa.
Katika mtandao wa TikTok, Akothee alifurahia baada ya mashabiki wake kumpa zawadi mbalimbali zikiwemo maua na hata simba – ambayo inatajwa kuwa zawadi yenye pesa nyingi kwenye jukwaa hilo la video fupi.
“Nimefurahi kuona jinsi mashabiki wangu wa TikTok walivyosherehekea siku yangu ya kuzaliwa! Asanteni nyote kwa upendo, burudani, vicheko, na zawadi. Sijawahi kupokea kiasi kikubwa cha shukrani na fadhili kama hizo. Nawapenda sasa hivi! 💕🙏 Asante sana kwa kila mtu kwa kuunga mkono Akothee Foundation. Mmeweka tabasamu kwenye uso wa mtu leo. Asante, asante, asante!” Akothee aliandika kwenye video hiyo akizawadiwa simba na jamii ya TikTok.
Kando na mashabiki kumpa zawadi, Akothee pia alifichua njia maalum ambayo mpenzi wake wa zamani Nelly Oaks na ambaye wametajwa kurudiana kinyemela, aliyotumia kumsherehekea.
Akothee alifichua kwamba Nelly Oaks alimsherehekea kwa njia ya kipekee kwa kulipia matangazo ya biashara kwenye mabango 3 makubwa ya barabarani kutangaza wakfu wake wa Akothee Foundation.
“Wee Nellyoaks ameamua. Wee Nellyoaks amefanya uamuzi wa kufurahisha. ❤️❤️❤️❤️Aliahidi mabango matatu kusaidia Wakfu wa Akothee. Kitendo hiki cha ukarimu kinagusa sana. Anajua moyo wangu uko pamoja na jamii. Tazama jinsi mume wangu amenisherehekea! Kwa vyombo vyote vya habari ambavyo vimenitakia maisha marefu, mbarikiwe. Kwa mashabiki wangu wote, asanteni sana kwa sapoti yenu isiyoyumba,” alisema.