Nana Owiti ajibu kwa nini alilazimika kuwavalisha wanawe kama Waislamu siku ya Eid

“Wanangu waliomba kuvaa hivyo leo kwa sababu rafiki yao Moha alikuwa na karamu. Inaonekana Moha hakutupa mwaliko huo wa Pilau kwa hivyo tukashughulikia. Walitaka pilau kutoka kwa Moha jamani,” Nana Owiti alisema.

Wanawe King Kaka na Nana Owiti
Wanawe King Kaka na Nana Owiti
Image: instagram

Nana Owiti, mke wa msanii King Kaka amejibu swali kutoka kwa mashabiki wake kuhusu ni kwa nini aliamua kuwavalisha wanawe wa kiume mavazi ya Kiislamu, jambo ambalo si la kawaida kwa familia yake.

Jumatano ilikuwa ni sikukuu ya kusherehekea kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa Waislamu.

Shereh hizo za Eid ul Fitr ziliandaliwa kote nchini katika misikiti mbalimbali, lakini vijana wa Nana Owiti licha ya kuwa Wakristu, walionekana kwenye kanzu na vilemba kama Waislamu.

Nana Owiti ndiye aliyepakia video hiyo na alilazimika kujieleza kwa baadhi ya mashabiki wake ambao waliuliza sababu ya mavazi hayo.

Kwa maelezo ya Owiti, wanawe walivaa hivyo kwa sababu ya rafiki yao kwa jina Moha, akitania kwamba walikuwa wanataka pilau.

“Wanangu waliomba kuvaa hivyo leo kwa sababu rafiki yao Moha alikuwa na karamu. Inaonekana Moha hakutupa mwaliko huo wa Pilau kwa hivyo tukashughulikia. Walitaka pilau kutoka kwa Moha jamani,” Nana Owiti alisema akimjibu mmoja aliyeuliza, Mbona hawa wamevaa kanzu 😂, kwa kawaida Huwa hawavai?”

Katika video hiyo, Owiti na wanawe walionekana kujivinjari kwa ziara za matembezi na kusema kwamba ilikuwa ni kumbukumbu nzuri ya kujirejesha katika maisha yake ya utotoni viungani mwa mto Tana.

“Niliipenda ile sehemu ndogo ya uvuvi kwa sababu nilikua karibu na R.Tana huko Mwea. Uvuvi ulikuwa jambo la kawaida huko. Wengine hata waliacha shule na kuwa wavuvi wadogo na wavuvi🤯.Nyumbani kwetu, Jumamosi zilikuwa siku za sherehe! Mjomba wangu marehemu Nganda na mjomba Ngei ndio wangevua samaki na kuleta samaki nyumbani kwani mjomba wangu Peter na Muya wangeenda kuwinda na mbwa na kuleta ‘tuvaluku’, ‘nthia’ na ‘ikanga’.”