Familia ya Nameless na Wahu Kagwi wana furaha baada ya binti yao mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 5 kung’amua kukariri kwa kuhesabu nambari moja hadi 10.
Wahu alijionea fahari kwa kitinda mimba wake na kupakia video hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram, akimtaja binti huyo kama mtoto mwerevu kupindukia.
Hata hivyo, msanii huyo hakuweza pia kujitapa akisema kuwa bla shaka werevu wa bintiye ni kama wa mama yake.
“Haka ni kerevu kama mama yake,” Wahu alisema.
Binti huyo aliyezaliwa mwezi Oktoba mwaka 2022 mpaka sasa ana miezi 17 lakini alionekana kuwa makini katika kuhesabu takwimu hizo ambazo aghalabu huwapa changamoto watoto wa umri wake.
Mashabiki wake walimpongeza kwa kazi kubwa katika malezi ya mtoto huyo.
Hizi hapa ni baadhi ya pongezi;
“Huyu mtoto amefikisha mwaka mmoja?...brilliant” mmoja aliuliza ambapo Wahu alijibu kwamba ana mwaka mmoja na miezi 5.
“Huyu atasoma jalada lote la katiba ya 2010 mwanzo hadi mwisho👏👏atakapofikisha miaka 3,” shabiki mwingine alisema.
“Mtaalamu wa hisabati, tunda halikuanguka mbali na wahu,” mwingine alisema.