Siku maiti itafufuka nitaacha kazi nirudi TikTok – Mfanyikazi wa mochari, Ann Mwangangi

"Aamke akienda?...Ikaeza fika point mtu aamke nikiwa job nakuja huku nitaptap screen, siwezi fanya hiyo kazi tena... Lakini ni ngumu sana maana tunaangalia pia kama haupo," Mwangangi alijibu.

Muhtasari

• Mwangangi ni tiktoker maarufu ambaye amekuwa gumzo katika mtandao wa tiktok kutokana na kudhaniwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na tiktok mwenza, Baba Talisha.

Ann Mwangangi
Ann Mwangangi
Image: instagram

TikToker anayejivunia kuwa mfanyikazi wa makafani, Ann Mwangangi amefunguka hatua atakazozichukua endapo siku moja mfu ataletwa mochwari kisha baadae afufuke.

Akizungumza kwenye kipindi cha mubashara na tiktoker mwenza, Hannah Benta, Mwangangi alisema kwamba japo hilo halijawahi tokea, lakini siku litamtokea akiwa kazini, hiyo itakuwa siku yake ya mwisho kufanya kazi ya kuwahudumia maiti.

Mwangangi alisema kwamba ni vigumu mtu amekufa afufuke kaitka makafani, lakini pia hakuweza kupuuzilia mbali uwezekano wa watu kufufuka, pengine wale wanaopelekwa mochari wakidhaniwa wamekufa kumbe wamepoteza fahamu.

"Hakuna siku hata moja ushawahi letewa mtu akaamka?" Hannah Benta alimuuliza Mwangangi.

"Aamke akienda?...Ikaeza fika point mtu aamke nikiwa job nakuja huku nitaptap screen, siwezi fanya hiyo kazi tena... Lakini ni ngumu sana maana tunaangalia pia kama haupo," Mwangangi alijibu.

Mwangangi ni tiktoker maarufu ambaye amekuwa gumzo katika mtandao wa tiktok kutokana na kudhaniwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na tiktok mwenza, Baba Talisha.

Mwagangi pia alimiminiwa pongezi na sifa baada ya kutajwa kuwa mmoja wa watu waliohudumia maiti ya tiktoker marehemu, Brian Chira.