Mjasiriamali Akothee ameonekana kurejea katika mtandao wa TikTok na kimbunga cha aina yake, miezi kadhaa baada ya kupapurana na tiktoker Nyako katika mtandao huo wa video fupI.
Akothee ambaye yuko katika harakati za kufanya hafla kubwa ya kufanikisha mradi wake wa Akothee Foundation hivi karibuni alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na kuwaomba mashabiki wake kuendelea kuchangia wakfu huo kwa ajili ya kusaidia watoto kutoka familia zisizojiweza kupata elimu.
Katika mtandao wa TikTok, Akothee amekuwa akifanya vipindi vya mubashara kujumuika na mashabiki wake ambao wamekuwa wakimsherehekea kwa kumtumia zawadi ainati zenye thamani mbalimbali kwenye jukwaa hilo.
Msanii huyo alifichua kwamba mpaka sasa tayari mashabiki wake kwenye TikTok wamemheshimisha kwa kumpa zawadi za simba 9 – zinazotajwa kuwa zawadi za thamani ya juu, huku pia akifichua kwamba katika bara la Afrika wamemfanya kuwa katika nafasi ya 3 kwa watu waliokwenda live na kuwa na uungwaji mkono wa umati mkubwa.
Kando na zawadi za simba, Akothee pia alifichua kwamba amepewa zawadi mbalimbali zikiwemo pesa, treni, ndege – zote zenye thamani tofauti na jumla ni nusu milioni.
“TWENDENI TIKTOK kuna Mambo ya kuvutia sana. Tazama jinsi mashabiki wangu wa TikTok walivyosherehekea siku yangu ya kuzaliwa 🙏 na kuunga mkono Akothee Foundation 💪🙏 👏👏👏👏👏👏👏MWANAMKE WA KWANZA WA KENYA KUPIGA NO, Popular Live namba 3 barani Afrika, Ligi C2 kwenye nambari 1, Taji, Cheo cha Wiki kwa nambari 9. Na simba 9, ulimwengu 1, nyangumi, kogis, sarafu, ndege, treni na pesa,” Akothee alisema huku akiwashukuru mashabiki.
Hata hivyo, licha ya kusherehekea, baadhi ya mashabiki walimrudisha nyuma kipindi anagombana na Nyako na kumkumbusha kwamba aliwahi sema TikTok ni ya watoto.
Akothee alijibu akisema kwamba huo ulikuwa ni mzaha na kuwaomba mashabiki wake wa TikTok kuendelea kuchangia kwa ajili ya Akothee Foundation.
“Nakumbuka ulikuwa ukisema tiktok ni ya watoto na mwishowe uko hehe,,, never say never in life.” Cay KJ alimkumbusha.
“because you don't get my jokes trust me at your own risk , sasa unatakaje?” Akothee alimjibu.