Obinna amnunulia Dem wa FB simu ya iPhone 13 pro max kupitia ‘Lipa Mdogo Mdogo’

"Niliwaza kwamba ndio ninaweza amua na nimnunulie simu hiyo lakini nilitaka nyinyi mashabiki wake mshukuru kwa kazi nzuri anayowafanyia, kwa hiyo tuje pamoja kama familia na kumnunulia simu,” Obinna alieleza.

Muhtasari

• Obinna pia alieleza sababu ya kutumia njia ya michango kumnunulia Dem wa FB simu licha ya kuwa na uwezo wa kumnunulia simu hiyo bila kuchangisha hela kutoka kwa watu.

 

Oga Obinna amnunulia Dem wa FB simu
Oga Obinna amnunulia Dem wa FB simu
Image: Screengrab//YouTube

Mchekeshaji chipukizi, Dem wa FB ni mwenye furaha baada ya bosi wake, YouTuber Oga Obinna kumnunulia simu ya iPhone.

Kupitia kipindi cha Obinna Live kwenye YouTube, Obinna alim’surprise na simu ya iPhone 13 pro max Dem wa FB ambaye katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakishirikiana kwenye chaneli hiyo kukuza maudhui.

Obinna alieleza kwa nini aliamua kumchukulia Dem wa FB simu kupitia mpango wa malipo ya pole pole, akisema kwamba hivi majuzi waliandaa kipindi cha mubashara kwenye TikTok akiwaomba mashabiki wake kumchangia Dem wa FB kununua simu hiyo ya ndoto yake, wengi walimtupia matusi.

“Katika kipindi cha wiki moja imepita, tumekuwa tunachanga pesa ili kumnunulia Dem wa FB simu. Kwa sasa tumefikisha 77k ili kumnunulia simu, tulifanya ‘live session’ ambayo tulitukanwa lakini hatutaacha kuchanga,” Obinna alisema.

Obinna pia alieleza sababu ya kutumia njia ya michango kumnunulia Dem wa FB simu licha ya kuwa na uwezo wa kumnunulia simu hiyo bila kuchangisha hela kutoka kwa watu.

 “Tumepata watu wengi ambao wako tayari kwa michango yao. Ahsanteni sana na tunashukuru sana na jana ilinijia kwamba nilikuwa natumia njia mbaya kupata simu. Sababu iliyonifanya kufanya hivyo [kuchangisha] ni kwamba Dem wa FB anawaburudisha, ni mtu wenu. Na niliwaza kwamba ndio ninaweza amua na nimnunulie simu hiyo lakini nilitaka nyinyi mashabiki wake mshukuru kwa kazi nzuri anayowafanyia, kwa hiyo tuje pamoja kama familia na kumnunulia simu,” Obinna alieleza.

Baada ya kutukanwa, Obinna alifichua kwamba baadae walipata watu wengi ambao walitaka kumsaidia Dem wa FB kupata simu ya iPhone, na kwenda mbele kueleza jinsi alifanikisha hilo kabla ya kumkabidhi mrembo huyo simu yake kwa furaha.

“Ila sasa niko na marafiki zangu kutoka duka la kuuza iPhone ya malipo ya pole pole. Kwa hiyo unachanga pole pole, na tulizungumza nao kupitia njia ya simu na hivyo ndivyo tulivyopata simu,” Obinna alisema huku akimfungulia Dem wa FB kifurushi cha simu yake ya iPhone 13 pro max.