logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nyota Ndogo atangaza azma ya kufanya kolabo ya Hip Hop na wasanii wa Pwani

“Tuimbeni tu tumepewa vipaji tusikate tamaa...nitakusanya pesa zangu za chapati tufanye video.”

image
na Davis Ojiambo

Burudani22 April 2024 - 14:26

Muhtasari


  • • Nyota Ndogo ni mmoja kati ya wasanii wa kitambo ambao walifana kipindi hicho na wimbo wake ‘Watu na viatu’.
  • • Katika siku za hivi karibuni, Nyota Ndogo amekuwa akipaza sauti kuhusu matatizo yanayomkumba msanii Stevo Simple Boy.
NYOTA NDOGO

Msanii kutoka upande wa Pwani ya Kenya, Nyota Ndogo ameweka wazi azma yake ya kuwashika mkono wasanii wa rap kutoka sehemu hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Nyota Ndogo alisema kwamba licha ya kuwa msanii wa kizazi cha zamani, bado anatamani kufanya angalau kolabo chache na wasanii wa Hip Hop kutoka Pwani.

“Najua mimi ni zilipendwa lakini nitafurahi nikifanya nyimbo moja na wasanii wa nyumbani Mombasa wa HIP HOP. Kilifi moja kuvuka Likoni moja Mombasa moja tana moja malindi moja.tutatoshea kwa nyimbo moja?” Nyota Ndogo alisema.

Mjasiriamali huyo wa mgahawa wa vyakula aina ya chapati aliwatoa wasiwasi wasanii wa HipHop kuhusu video akisema yuko tayari kutumia hata akiba ya mapato kutoka kwa uuzaji wa chapatti zake kwa ajili ya kurekodi video.

“Tuimbeni tu tumepewa vipaji tusikate tamaa...nitakusanya pesa zangu za chapati tufanye video.”

Nyota Ndogo ni mmoja kati ya wasanii wa kitambo ambao walifana kipindi hicho na wimbo wake ‘Watu na viatu’.

Katika siku za hivi karibuni, Nyota Ndogo amekuwa akipaza sauti kuhusu matatizo yanayomkumba msanii Stevo Simple Boy.

Alisema kwamba alikuwa anatafuta namba ya msanii huyo wa Kibera ili kumshika mkono, akisema kwamba msaada aliokuwa nao ni kumsaidia Stevo kurudi shule angalau kupata elimu ya kujua kusoma na kuandika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved