logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hatimaye Rihanna amebadilisha picha ya utambulisho wake Instagram baada ya miaka 10

Mwishoni mwa juma, mashabiki waligundua kuwa RiRi alibadilisha picha yake ya wasifu.

image
na Radio Jambo

Habari23 April 2024 - 06:39

Muhtasari


• Shabiki mmoja alitweet, "Rihanna akibadilisha instagram pfp yake ya kitambo na kuweka bidhaa ya fenty… sasa hapa ndipo tunaweka mstari."

RIHANNA abadilisha picha

Hatimaye Rihanna amebadilisha picha yake ya wasifu kwenye Instagram kwa mara ya kwanza katika kipindi cha muongo mmoja.

Wiki iliyopita, picha ya kichwa cha mdoli yenye nywele imekuwa kama utambulisho wake Instagram kwa miaka 10 iliyopita lakini juzi usiku ameibadilisha na picha ya mkono unaoshikilia bidhaa inayosadikika kuwa ya Fenty Beauty ufukweni.

Mwishoni mwa juma, mashabiki waligundua kuwa RiRi alibadilisha picha yake ya wasifu kwenye Instagram kiujanja kutoka kwa doodle ya kifimbo ambayo amekuwa nayo kwa miaka 10 iliyopita.

Badala yake, ukurasa wa mkali huyo wa Diamonds, sasa unaangazia mkono wa umbo la fimbo ulioshikilia bidhaa ya Fenty kwenye mandharinyuma ya machweo.

Ingawa picha hiyo ni promosheni ya safu ya bidhaa za urembo za RiRi, mashabiki walienda kwa X na "kuomboleza" sura ya doodle ambayo imekuwapo kwa muongo mmoja huku wengine wakichukua mabadiliko kama ishara kwamba bilionea huyo hatatoa muziki wowote mpya tena hivi karibuni.

Shabiki mmoja alitweet, "Rihanna akibadilisha instagram pfp yake ya kitambo na kuweka bidhaa ya fenty… sasa hapa ndipo tunaweka mstari."

Mtumiaji mwingine aliandika, "Rihanna amebadilisha picha yake ya wasifu kuwa bidhaa ya urembo ... KAMWE hatupati muziki mpya."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved