“10k kwa dakika moja!” Jackie Matubia aweka wazi rate-card ya kutangaza biashara

Kwa sekunde 15 pekee, Matubia aliweka wazi kuwa lazima alipwe shilingi 2,500 huku sekunde 60 sawa na dakika moja akiweka kiwango chake kuwa shilingi elfu 10 ili kufanya tangazo.

Muhtasari

• Mama huyo wa mabinti wawili aliwashangaza watu baada ya kufichua kwamba viwango vyake huenda na muda wa sekunde tu.

Image: INSTAGRAM/ JACKIE MUTUBIA

Muigizaji nguli Jackie Matubia ameweka wazi kiwango cha pesa anazodai ili kufanya tangazo la kibiashara.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Matubia alichapisha viwango mbalimbali na muda sawia kulingana na urefu wa tangazo na kuwaomba wafanyibiashara wanaotaka kuongeza mauzo ya bidhaa au huduma zao kumfuata kupitia barua pepe ili kumpa kazi ya kuwatangazia biashara zao.

Mama huyo wa mabinti wawili aliwashangaza watu baada ya kufichua kwamba viwango vyake huenda na muda wa sekunde tu.

Kwa sekunde 15 pekee, Matubia aliweka wazi kuwa lazima alipwe shilingi 2,500 huku sekunde 60 sawa na dakika moja akiweka kiwango chake kuwa shilingi elfu 10 ili kufanya tangazo.

“Jamani tushirikiane! Wasiliana kupitia simu au barua pepe," alisema wakati akishiriki maelezo ya tangazo kwenye mitandao yake ya kijamii.

"Sekunde 15 Ksh 2,500, sekunde 45 Ksh 4,000 na sekunde 60 Ksh 10,000," mama huyo wa watoto wawili aliweka viwango vyake hadharani akiwafahamisha jinsi ada zake zinavyofanya kazi ikiwa wangetaka.

Image: instagram matubia jackie

Matubia aliweka haya wazi ikiwa ni siku chache baada ya kuweka rekodi ya kuwa mwigizaji wa kwanza wa kike kufanikisha kuonyeshwa kwa filamu yake ya mfululizo kwenye mtandao inayoitwa ‘Toxic’ kupitia YouTube.

Matubia ni muigizaji wa muda mrefu tangu enzi za Tahidi High, kipindi kilichokuwa kinaruka kila wiki kwenye runinga ya Citizen kabla ya kuibuka tena katika ukubwa wake kwenye filamu nyingine ya Zora kwenye runinga hiyo akiigiza kama ‘Nana’.

Kwenye kipindi hicho, Matubia ndipo walikutana na muigizaji mwenza Blessing Lung’aho aliyekuwa akiigiza kwa jina ‘Madiba’ kabla ya kuchipuka kwa penzi lao na pamoja wakabarikiwa na binti lakini uhusiano wao haukuweza kudumu Zaidi ya miaka miwili.

Kwa sasa, Matubia anasema hana mpango wa kujaribu bahati katika ndoa tena bali analenga Zaidi kuwawekea mabinti zake maisha mazuri ya mbeleni.