Cassypool aeleza kwa nini Ringtone anastahili kuheshimika Kenya

"Injili ya kisasa ya Kenya imeshikiliwa na Ringtone kama mwenyekiti, yeyote anayejidai kuwa mwenyekiti mbadala ni takataka. Ringtone ndiye mwenyekiti pekee,” Cassypool alichemka

Muhtasari

• Cassypool alisema ni wakati sasa Wakenya wajirudi katika misingi yao, akisema hili taifa huko nje linajulikana kama taifa la wachamungu wahafidhina.

Cassypool baada ya kurejea kutoka ziara ya Ulaya, ameweka wazi kwamba alichojifunza huko nje kuhusu Kenya ni kwamba ni taifa liilosimikwa katika misingi ya injili.

Alimshukuru msanii wa injili Bunny Asila kwa kufadhili ziara yake ambapo alisema alimwezesha kutembelea mataifa Zaidi ya 10 Ulaya.

Cassypool alisema ni wakati sasa Wakenya wajirudi katika misingi yao, akisema hili taifa huko nje linajulikana kama taifa la wachamungu wahafidhina.

“Nilichojifunza huko Ulaya ya kwamba Kenya ni nchi ya Injili, hii sio nchi ya watu wanaokuja kusema eti tunaimba sekula, hili ni taifa liilojengwa kwa misingi ya injii. Rais wa nchi, mkewe na hata familia ya naibu rais wote wanapenda injili, mbona wewe mtu wa kawaida usipende injili?” Cassypool aliuliza.

Cassypool pia alimpa maua yake Bunny Asila, akisema kuwa amefanikiwa kutangaza injili ya Kenya huko Ulaya huku pia nchini akisema Guardian Angel na Ringtone wanastahili heshima zao kwa kiwango kikubwa.

“Guardian Angel ni msanii wa injili namba moja Kenya, na lazima tumtambue hivyo na kumheshimu. Na lazima tuheshimu Ringtone kama mwenyekiti wa wasanii wa injili Kenya nzima. Injili ya kisasa ya Kenya imeshikiliwa na Ringtone kama mwenyekiti, yeyote anayejidai kuwa mwenyekiti mbadala ni takataka. Ringtone ndiye mwenyekiti pekee,” Cassypool alichemka.

Cassypool alisema kuwa atampeleka Bunny Asila kwa Ringtone na kumtaka kunyenyekea kwake kwani huyo ndiye mwenyekiti kabla ya kuanza mipango mingine yoyote ya kuratibu ziara ya kutangaza injili ya Kenya katika mataifa mbalimbali duniani.