“Huyu kijana ni mtanashati, hata mimi nitaanza kuendesha pikipiki” – Kanyari amsifia Tizian

"Huyu kijana ni mrembo aki, ni mtanashati. Hata mimi nitatengeneza nywele, niwe nakaa vizuri na pikipiki. Tizian na mimi nitaanza kuendesha pikipiki juu yako.," Kanyari alisema

Muhtasari

• “Mtu anasema anataka kuongea na Kanyari, wewe kuja na milioni moja kama unataka mahojiano. Na kama unataka kuniuliza mambo ya 310 ni sawa,” Kanyari alisema.

Pasta Kanyari na Tizian Savage
Pasta Kanyari na Tizian Savage
Image: Maktaba

Mchungaji Victor Kanyari amemmiminia sifa tiktoker King Tizian Savage baada ya kumtumia zawadi ya pesa.

Kanyari ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akifanya vipindi vya mubashara kwenye mtandao wa TikTok akihubiri na kuwaomba wafuasi wake kumtumia zawadi, alimsifia Tizian akisema kwamba ni mtanashati kupindukia.

Tizian, mwanabodaboda aliyepata umaarufu kwenye TikTok kutokana na kile wafuasi wake wanasema ni utanashati wa kipekee alishikwa mkono na kuanza kuunda maudhui kwenye mtandao huo wa video fupi na marehemu Brian Chira.

Baada ya kumtumia Kanyari zawadi ya pesa, Mchungaji huyo alimsifia kwa utanashati wake akisema kwamba kijana huyo anamchochea kutaka kusuka nywele za rasta kama yeye na hata kuanza kuendesha pikipiki, akisema kuwa watu wanampenda sana.

“Mungu akubariki Tizian rafiki yangu bora Zaidi, ooh Mungu wangu napenda huyu kijana. Huyu kijana ni mrembo aki, ni mtanashati. Hata mimi nitatengeneza nywele, niwe nakaa vizuri na pikipiki. Tizian na mimi nitaanza kuendesha pikipiki juu yako. Mimi sikuwa najua watu wa pikipiki mnapendwa namna hiyo,” Kanyari aisema.

Mchungaji huyo pia alikwenda mbele na kumsifia kijana huyo kwa pongezi za kununua gari lake la kwanza baada ya kuvuma TikTok kwa muda mfupi.

“Kusema ukweli muwe mnaheshimu watu, kijana ametoa kusikojulikana, amepiga hustle yak hapa TikTok sasa hivi ni mtu mkubwa anaendesha Audi na alitoka kwa pikipiki,” Kanyari aliongeza.

Mchungaji huyo aliwasuta watu ambao wanamuita mkora na wakati huo huo wanataka kufanya mahojiano na yeye.

Kanyari alisema mtu yeyote anayetaka kuzungumza naye kuhusu mbegu ya 310, sadaka maarufu aliyokuwa akiomba kwenye kanisa lake kabla ya kuanikwa na Jicho Pevu, lazima mtu huyo amtafute na shilingi milioni moja.

“Mtu anasema anataka kuongea na Kanyari, wewe kuja na milioni moja kama unataka mahojiano. Na kama unataka kuniuliza mambo ya 310 ni sawa,” Kanyari alisema.