Crown FM itacheza nyimbo za Diamond na Harmonize bila kubagua - Alikiba

"Nilipokuwa nikiifungua media yangu nikasema hii ni ya kila mtu na si ya familia. Crown fm itacheza nyimbo za Diamond na Harmonize bila kubagua. Natamani pia Wasafi Media wafanye hivyo kwa wasanii wengine,” Alikiba.

Muhtasari

• Itakumbukwa wiki chache zilziopita katika mahojiano, Diamond alimkingia Alikiba kifua dhidi ya madai kwamba media ya Crown si ya kwake.

• Msanii huyo alizama Zaidi na kutaja majina akisema Crown FM itaendelea kucheza ngoma za Diamond na Harmonize bila kubagua.

 

mwaliko wa Diamond.
Alikiba amekataa mwaliko wa Diamond.
Image: INSTAGRAM

Msanii wa Bongo Fleva na mjasiriamali katika chombo cha habari cha Crown Media, Alikiba amefunguka sababu za stesheni yake ya redio inacheza ngoma hadi za washindani wake.

Crown FM ilianza kuenda hewani siku chache zilizopita na baadhi ya mashabiki wake kindakindaki walionekana kutofurahishwa mitanaoni baada ya ngoma za washindani wake kutoka lebo ya Wasafi kusikika zikichezwa kwenye redio hiyo.

Baadhi ya hao waliteta wakisema ngoma kama za Diamond Platnumz hazifai kuchezwa kwenye Crown FM kwa kile wanadai kwamba ngoma za wasanii kutoka Kings Music haswa Alikiba hazijawahi chezwa kwenye stesheni ya Wasafi FM.

Hata hivyo, Alikiba amekuja kufafanua akisema kuwa Crown FM haitabagua ngoma za msanii yeyote kwani ni media ya kila mtu.

Msanii huyo alizama Zaidi na kutaja majina akisema Crown FM itaendelea kucheza ngoma za Diamond na Harmonize bila kubagua.

Alikiba alikwenda mbele na kumuomba mkurugenzi wa Wasafi Media, Diamond kuhakikisha kuwa pia media yake haibagui wasanii na kuwapa muda wa kuchezwa ngoma zao kwa usawa.

Juzi nilifurahi sana baada ya kuona redio yangu ikicheza nyimbo za Diamond Platnumz. Ndio maana nilipokuwa nikiifungua media yangu nikasema hii ni ya kila mtu na si ya familia. Crown fm itacheza nyimbo za Diamond na Harmonize bila kubagua. Natamani pia Wasafi Media wafanye hivyo kwa wasanii wengine,” Alikiba alisema.

Itakumbukwa wiki chache zilziopita katika mahojiano, Diamond alimkingia Alikiba kifua dhidi ya madai kwamba media ya Crown si ya kwake.

Diamond alisema kuwa ni wakati umefika msanii yeyote mwenye uwezo kuzindua kituo cha habari kama njia moja ya kuhamasisha jamii.

Diamond alisema kwamba dhana ya kizamani kuwa usanii ni uhuni inafaa kubadilishwa katika akili za watu kupitia kwa kuwaonyesha kuwa usanii ni kazi ambayo inaweza ikampa mtu hela za kuwekeza katika miradi mikubwa kama chombo cha habari.