Jose Chameleone afichua kwa nini amepungua uzani wa mwili na kuharibika ngozi ya uso

Wakati video zinazomuonyesha Jose Chameleone akiwa katika hali mbaya zilipoibuka, watu wengi walihusisha hali yake na kunywa pombe kupita kiasi, kutengana na mkewe, na mafadhaiko miongoni mwa mengine.

Muhtasari

• Hata hivyo, Chameleone anasema alianza kupungua uzani kwa kasi baada ya kuacha kutumia nyama ya nguruwe.

• “Kuna mtu aliuliza anakula nini Chameleone, niliacha kula nyama ya nguruwe,” alisema hitmaker huyo wa Valu Valu. "Ndio maana nilikuwa na shida kidogo."

JOSE CHAMELEONE
JOSE CHAMELEONE
Image: Instagram

Msanii mwenye ufanisi mkubwa kimuziki kutokea Uganda, Jose Chameleone hatimaye amelizungumzia suala la mabadiliko katika mwili wake ambayo yamekuwa yakiwatia wasiwasi kwa muda mashabiki wake.

Chameleone kwa mara ya kwanza aliweza kuzungumzia kasi ya kupungua kwa uzani wa mwili wake lakini pia kubadilika kwa ngozi ya uso wake ambapo alionekana kuwa hayuko sawa kiafya.

Wakati video zinazomuonyesha Jose Chameleone akiwa katika hali mbaya zilipoibuka, watu wengi walihusisha hali yake na chaguzi tofauti za maisha, ikiwa ni pamoja na kunywa pombe kupita kiasi, kutengana na mkewe, na mafadhaiko miongoni mwa mengine.

Hata hivyo, Chameleone anasema alianza kupungua uzani kwa kasi baada ya kuacha kutumia nyama ya nguruwe.

“Kuna mtu aliuliza anakula nini Chameleone, niliacha kula nyama ya nguruwe,” alisema hitmaker huyo wa Valu Valu. "Ndio maana nilikuwa na shida kidogo."

Wakati huohuo, Chameleone alifichua hayo alipokuwa akitumbuiza kwenye onyesho ambalo pia alieleza kwanini anachaji zaidi ya kawaida kwa tamasha lake lijalo.

Watu wanauliza kwa nini ninatoza $100 (takriban Sh 13k)," alisema Chameleone kwenye video iliyoonekana na mwandishi wa habari hii.

"Unataka kuona vitu unavyoviona kwenye show za Davido lakini umelipa 700 pekee. Wewe kama shabiki, lipa zaidi ili msanii pia afanye mambo mazuri zaidi."

Mkali huyo wa ‘Tubonge’ alitangaza tamasha lake mwezi Februari.

Onyesho hilo lililopewa jina la 'Legends in Gold: We Love Chameleone', linatazamiwa kufanyika Agosti 31.

Kiingilio kitakuwa kati ya dola 100 hadi dola 3000.

Jose Chameleone katika mahojiano ya runinga, alitetea kipindi hiki cha bei akisema kinastahili jina lake na kile amefanya kwa tasnia ya muziki.