Kisa warembo kuvaa vibaya kwa gym, jamaa aacha mazoezi na kuzingatia safari ya mbinguni

Aliwaomba hadharani wanawake wanaohudhuria gym kuvalia kwa heshima, akisisitiza kwamba mwenendo unaoongezeka wa uvaaji usio na heshima katika mazingira kama hayo unasumbua na kuwatatiza wanaume kifikira.

Muhtasari

• Matokeo yake, Uchemba alisema kuwa hao ndio chanzo kilichosababisha yeye kukoma kuacha kushiriki mazoezi na kuacha kuzingatia safari yake ya kurithi ufalme wa mbinguni.

Muigizaji wa Nollywood, Uchemba Williams
Muigizaji wa Nollywood, Uchemba Williams
Image: Instagram

Muigizaji na muongozaji wa filamu za Nollywood kutokea Nigeria, Williams Uchemba, amefichua sababu ambayo ilimfanya kuacha kushiriki mazoezi kwenye gym za umma.

Uchemba katika video moja kwenye ukurasa wake wa Instagram, alinyoosha kidole kwa wanawake wanaoshiriki mazoezi kwenye gym za umma, akisema kuwa mavazi yao si ya adabu na heshima hata kidogo.

Matokeo yake, Uchemba alisema kuwa hao ndio chanzo kilichosababisha yeye kukoma kuacha kushiriki mazoezi na kuacha kuzingatia safari yake ya kurithi ufalme wa mbinguni.

Muigizaji huyo alitaja vishawishi vinavyotokana na mavazi hayo na kusema kwamba angeendelea kufanya mazoezi kwenye gym za umma angepotoka hivyo akaonelea ni heri kuasi gym na kuzingatia safari yake ya kiroho.

Katika kukabiliana na suala hilo, Uchemba amechukua hatua ya kuanzisha gym nyumbani ili kudumisha utimamu wake bila kukumbana na kero hizo.

Muigizaji huyo wa Nollywood anawaomba hadharani wanawake wanaohudhuria gym kuvalia kwa heshima, akisisitiza kwamba mwenendo unaoongezeka wa uvaaji usio na heshima katika mazingira kama hayo unasumbua na kuwatatiza wanaume kifikira.

Akitumia mtandao wake wa kijamii, Uchemba alizungumzia suala hilo moja kwa moja, akiwataka wanawake kutafakari upya uchaguzi wao wa mavazi kwa minajili ya kuzingatia wanaume wanaokwenda gym na ustawi wa kiroho.

"Wanawake, wanaume wote wanapaswa kuacha kuja kwenye mazoezi? Kwa sababu mavazi yanu yasiyo ya heshima yanatoka mkononi. Inakuwa ya kutisha. Nimechoka," alielezea.

Aliendelea, "Tafadhali, jaribuni kuvaa mavazi ya heshima kwenye mazoezi. Wanaume wengine wamedhamiria kujikita katika safari ya mbinguni, tafadhali msitusumbue. Kila mtu anapokuja kwenye mazoezi, analazimika kuona kile ambacho hakukusudia kukiona."

Alisisitiza kujitolea kwake kudumisha mtindo wa maisha unaozingatia kiroho, hata ikiwa ilimaanisha kujitolea kwa urahisi wa ukumbi wa mazoezi ya umma.

"Nyie wanawake mmejipanga kuwazuia wanaume wasiende mbinguni lakini haitafanya kazi kwa sababu nimetoka gym, nimeweka gym nyumbani kwangu kwa sababu siwezi kustahimili, nataka kufuata safari ya mbinguni,” alihitimisha.