Wazee wa jamii ya Agikuyu wafanya matambiko katika kaburi la Brian Chira (video)

"Hakutakuwa na chochote kuhusiana na LGBTQ, mashoga, usagaji na matumizi mabaya ya dawa za kulevya ambazo zingeibuka tena katika eneo hili. Kama wazee, tunabomoa roho zote zinazohusiana na LGBTQ kutoka eneo hili,” Wazee walilaani.

Muhtasari

• Marehemu Brian Chira alikumbana na kifo chake cha ghafla kupitia ajali iliyompata na kufariki papo hapo.

• Kufuatia kifo chake, marehemu alihusishwa na mambo mengi maovu yanayohusishwa na LGBTQ.

Brian Chira
Brian Chira
Image: Screengrab

Wazee wa jamii ya Agikuyu wamefanya matambiko katika boma na kaburi la marehemu TikToker, Brian Chira, mwezi mmoja baada ya maziko yake.

Katika klipu ya video iliyorekodiwa, wazee wa kijiji walifurika nyumbani kwa kina Brian Chira siku ya Alhamisi kusafisha na kulaani roho ya kitu chochote kinachohusiana na mapenzi ya jinsia moja, LGBTQ.

Kwenye video hiyo, wazee hao walionekana wamevalia mavazi ya kitamaduni na walionekana kuzunguka katika boma hilo na hadi kwa kaburi lake wakitamka maneno kwa lugha ya Agikuyu.

Walisema kwamba walikuwa wanasafisha boma na kijiji kwa jumla dhidi ya roho za LGBTQ.

"Hakutakuwa na chochote kuhusiana na LGBTQ, mashoga, usagaji na matumizi mabaya ya dawa za kulevya ambazo zingeibuka tena katika eneo hili. Kama wazee, tunabomoa roho zote zinazohusiana na LGBTQ kutoka eneo hili,” Wazee walilaani.

Baada ya shughuli hiyo ya utakaso wazee hao waliwashauri vijana kuamini mchakato huo wa kutafuta mali kwa kuepuka pesa za haraka zinazoweza kuwasababishia kifo.

“Wanarubuni ni wengi sana na tumeona watu wengi wakija mkoani hapa kuwajulisha kilichotokea kwa Brian Chira kuhusu fedha na mazishi ya watu maarufu, lakini tumeharibu madhabahu zote mbaya zilizoletwa hapa.”

"Tunataka kuwaambia vijana kwamba chochote kilichotokea katika eneo hili la Githunguri kilikuwa kibaya na kufuatia kisa hicho, wanaume huko Githunguri walijipanga kusafisha eneo hilo kupitia mila na tamaduni za Kikuyu ili kuhakikisha eneo hilo ni safi dhidi ya roho za LGBTQ," Waliongeza.

Marehemu Brian Chira alikumbana na kifo chake cha ghafla kupitia ajali iliyompata na kufariki papo hapo.

Kufuatia kifo chake, marehemu alihusishwa na mambo mengi maovu yanayohusishwa na LGBTQ.

Uhusiano huo ulishuhudiwa kwenye kaburi lake ambapo vijana walirekodiwa wakimimina pombe haramu kaburini, wengine wakikaribia kuvua nguo huku wengine wakipiga porojo.

Hilo liliwakera wazee wa kijiji waliopanga kufanya ibada na ibada ya kutakasa kulaani roho za LGBTQ katika eneo hilo. eneo.