Zari amshabikia mwanawe wa kiume, Prince Nillan kuiga babake Diamond kwa densi ya ‘Shu!’

Zari ambaye alikuwa anamrekodi video hiyo alisikika akimshabikia kwa vifijo huku kijana akijikaza kurusha mikono, na kugeuza macho kama baba yake kwenye video hiyo ya Shu!

Muhtasari

• Zari ambaye alikuwa anamrekodi video hiyo alisikika akimshabikia kwa vifijo huku kijana akijikaza kurusha mikono, na kugeuza macho kama baba yake kwenye video hiyo ya Shu!

Waswahili wanasema tunda huwa halidondoki mbali kutoka kwa mti uliolizaa.

Prince Nillan, mwanawe Zari Hassan na msanii Diamond Platnumz mwenye umri wa miaka saba ameonesha kuwa yuko katika nafasi nzuri ya kuvivaa viatu vya babake pindi atakapostaafu muziki.

Nillan, katika video ambayo imekuwa gumzo mitandaoni, alionekana akicheza densi ya wimbo wa Shu! Ambao ni kolabo ya babake Diamond na msanii Chley.

Nillan alikuwa na wanafamilia wengine, akiwemo mamake, Zari ndani ya gari wakati walimchezea wimbo huo na ghafla mtoto akasimama na kuanza kusakata densi, akiiga minenguo na staili za kucheza densi za babake.

Zari ambaye alikuwa anamrekodi video hiyo alisikika akimshabikia kwa vifijo huku kijana akijikaza kurusha mikono, na kugeuza macho kama baba yake kwenye video hiyo ya Shu!

“Eeeyi babaa. Twende nalo. Vibes nzuri. keti baba. Nimeipenda hii” Zari Hassan alimpigia makofi mwanawe kwenye video hiyo ya mtandaoni iliyosambazwa mtandaoni.

Kutoka kwa video inayoanzia kwenye kanuni ya mavazi, mtindo wa kucheza na urembo wa nywele, ni dhahiri kwamba Prince Nillan angechukua nyayo za baba yake katika safari yake ya muziki.

Tofauti na watoto wengi ambao mara chache hufuata kazi ya baba yao, Diamond Platnumz anaonekana kuwa mshauri na mfano wa kuigwa kwa watoto wake katika safari yake ya muziki.

Kando na Nillan, pia mwanawe Tanasha Donna, Naseeb Junior ameonekana kuiga nyayo za babake katika mavazi, mtindo wa nywele na kucheza piano.