Diamond akubali kushindwa na Harmonize katika majibizano,“mimi mnyonge, chukua tu ushindi!”

“Oooh, kumbe una dhamira ya kubishana. Mimi ni mnyonge siwezi kubishana na wewe mtu mzito. Mataji yote nakupa chukua ushindi,” Diamond alisema.

Muhtasari

• Harmonize akijibu kauli hiyo ya kuachiwa ushindi, alisema Diamond ndiye mshindi kwa vile anasema alimtoa kimuziki.

• Harmonize pia alikiri kujibu kwamba anakaribia kujuta wakati ni ukweli Diamond ana kila haki na kujivunia kumtoa kimuziki.

Diamond na Harmonize
Diamond na Harmonize
Image: Facebook

Saa chache baada ya Harmonize kumkaripia kwa mipasho aliyekuwa bosi wake, Diamond Platnumz kisa kauli zake za mara kwa mara kwamba yeye ndiye chanzo cha mafanikio ya Harmonize kimuziki, Diamond amemjibu akionekana kujitenga mbali na malumbano ya mitandaoni.

Juzi-kati, Diamond alirejelea kwamba daima Harmonize na Rayvanny watasalia kuwa wanawe na atazidi kujivunia mafanikio yao kimuziki, akisema kuwa bila yeye, pengine hawangejulikana kimuziki.

Itakumbukwa Harmonize alikuwa msanii wa kwanza kabisa kusainiwa katika lebo ya WCB Wasafi iipozinduliwa 2015 kisha akaja Rayvanny na wengine kama Lava Lava, Queen Darleen na baadae Mbosso na Zuchu na mwaka jana akamalizia Dvoice.

Baada ya Diamond kusema hivyo, tamko hio lilionekana kutomfurahisha Harmonize ambaye alisema kauli za kusema kila mara kwamba alimsaidia zinachosha na kukera.

Harmonize alienda mbele na kuchomoa makombora ya maneno akiyalenga kwa kambi ya Diamond, kumwambia kwamba anakaribia kujuta kukubali msaada wake kimuziki lakini pia akamwambia kwamba aache kujivunia mafanikio yake kwani alishamlipa hela za kuvunja mkataba.

Kwa kumjibu, Diamond alionekana kukubali akisema kwamba hakuwa anajua Harmonize alikuwa amejitayarisha kwa malumbano.

Diamond alimwambia Harmonize kwamba ameshinda katika vita hiyo ya maneno akijitaja kama mnyonge ambaye hawezi tena kuendelea kubiashana.

“Oooh, kumbe una dhamira ya kubishana. Mimi ni mnyonge siwezi kubishana na wewe mtu mzito. Mataji yote nakupa chukua ushindi,” Diamond alisema.

Harmonize akijibu kauli hiyo ya kuachiwa ushindi, alisema Diamond ndiye mshindi kwa vile anasema alimtoa kimuziki.

Harmonize pia alikiri kujibu kwamba anakaribia kujuta wakati ni ukweli Diamond ana kila haki na kujivunia kumtoa kimuziki.

“Mshindi ni wewe kaka uliyenitoa. Tena najilaumu kwa nini nilijibu wakati bado ni hai yako kujivunia. Ni vile umejivunia sana hadi inachosha, na huwa unajivunia pale unapotaka huruma ya watu. Ila kisirisiri huku ukiwaambia waanaji wa shoo haswa za nje kwamba nikiwepo mimi Konde boy huwezi kufanya maana tutaonekana tupo kiwango sawa,” Harmonize alimwambia.