KRG aorodhesha sheria na masharti 8 magumu kwa marafiki na wanafamilia wake

“Usije kwa nyumba yangu kama hujaalikwa, sasa hivi tuna mbwa wapya na wanang’ata pia. Na kwa marafiki zangu za zamani poleni, niliwaachia pombe nikarudi kwa Mungu, kwa hiyo tukutane kwa nyumba ya maombi,” alimaliza.

Muhtasari

• Katika orodha hiyo, KRG aliorodhesha masharti 8 mapya ambayo alisema yataanza kufanya kazi mara moja kwa mtu yeyote anayehitaji msaada wake.

KRG
KRG
Image: FACEBOOK

Msanii wa dancehall KRG The Don ameorodhesha masharti magumu ambayo anadai yatakuwa yanafanya kazi kwa marafiki zake wa karibu pamoja na wanafamilia ambao wanahitaji uwepo wake katika maisha yao kwa njia moja au nyingine.

Kupitia insta story yake, KRG alisema kwamba anafurahia jinsi maisha yake ya kimuziki yanazidi kukolea akisema kwamba sasa inabidi afanyie marekebisho baadhi ya masharti haswa kwa watu ambao wanamuhitaji lakini pia wanafamilia.

Katika orodha hiyo, KRG aliorodhesha masharti 8 mapya ambayo alisema yataanza kufanya kazi mara moja kwa mtu yeyote anayehitaji msaada wake.

“Siku hizi nina furaha sana kuhusu Bughaa mpya. Yaani ile roho yangu nzuri siku hizi najua jinsi ya kudeal na baadhi ya watu ambao walikuwa na mazoea ya kuchukulia fursa ukarimu wangu kuwa udhaifu,” KRG alisema.

“Kama wewe ni rafiki yangu na hujawahi nisapoti kwa njia yoyote usijaribu kunipigia simu wakati unahitaji msaada wangu. Huwa nasaidia tu wale ambao wananisaidia, hapa Nairobi kila mtu ale kwa urefu wa Kamba yake. Kama hatuna biashara yoyote tunafanya pamoja, usijaribu kupiga namba yangu ya simu, nina marafiki wengi wa kutosha tayari,” KRG alianza kuorodhesha.

Msanii huyo pia aliweka wazi kwamba hapendi udaku, akishauri watu wanaosikia akisengenywa kuchangia katika kueneza umbea huo badala ya kurekodi na kumletea.

“Hata kama tunatoka familia moja na huwa hatuzungumzi kwa sana, wewe pia hufai kunipigia simu wakati una tatizo la kibinafsi. Bughaa hana huruma. Ukiwa na kitu cha maana kuniambia fuata taratibu zinazofaa kama wale wengine, si kurukia tu,” KRG aliongeza.

“Usije kwa nyumba yangu kama hujaalikwa, sasa hivi tuna mbwa wapya na wanang’ata pia. Na kwa marafiki zangu za zamani poleni, niliwaachia pombe nikarudi kwa Mungu, kwa hiyo tukutane kwa nyumba ya maombi ama tuombeane kutoka mbali,” alimaliza.