Edday Nderitu asherehekea mwaka mmoja tangu alipochukua uamuzi wa kijasiri kuhamia USA

“Ni mwaka mmoja uliopita leo nilipochukua hatua ya imani na kuanza ukurasa mpya katika maisha yangu! Hilo linahitaji ujasiri na uamuzi mwingi. Hapa ni kusherehekea ukuaji wangu," Edday alisema.

Muhtasari

• Mama huyo wa watoto watatu alisema amegundua nguvu mpya na maono mapya kuhusu uwezo wake ambao hakuwa amegundua hapo awali.

• Nderitu alisema kuwa ndoa yake ilikuwa imedumu kwa miaka 15 lakini akasisitiza kwamba hakuwa tayari kuendelea kuwalea wanawe katika ndoa yenye wake Zaidi ya mmoja.

EDDAY NDERITU
EDDAY NDERITU
Image: Facebook

Edday Nderitu, mke wa msanii wa Mugithi, Samidoh amesherehekea kuadhimisha mwaka mmoja tangu alipofanya maamuzi magumu na kufungua ukurasa wa safari ya matumaini kwa kuhamia Marekani baada ya panda-shuka nyingi kwenye ndoa yake.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Nderitu alisherehekea kipindi hicho cha mwaka mmoja akisema kwamba ilimchukua Imani ya kiwango cha hali ya juu kufanya uamuzi huo ambao kwa sasa hajutii na anafurahia maisha mbali na nyumbani.

Akisherehekea, Nderitu alifichua kwamba katika kipindi hicho, amejitambua na kukua kwa kiasi kikubwa.

“Ni mwaka mmoja uliopita leo nilipochukua hatua ya imani na kuanza ukurasa mpya katika maisha yangu! Hilo linahitaji ujasiri na uamuzi mwingi. Hapa ni kusherehekea ukuaji wangu, uthabiti, na matukio yasiyojulikana yaliyo mbele yangu!” Edday Nderitu alisema.

Mama huyo wa watoto watatu alisema amegundua nguvu mpya na maono mapya kuhusu uwezo wake ambao hakuwa amegundua hapo awali.

“Nimegundua uwezo mpya, nimeanzisha mikakati ya kukabiliana na hali hiyo, na kupata maarifa muhimu kunihusu na uwezo wangu. Nitandelea kusonga mbele, hata kama njia iliyo mbele bado haijaeleweka. Nimepata hii! Kumbuka kwamba kila hatua, hata zile zinazohisi kutokuwa na uhakika au za kutisha, ni fursa ya kukua na kujifunza,” alisema.

Nderitu aliondoka Kenya mwaka jana na wanawe wote kwenda USA baada ya kile aichokitaja kushindwa kustahimili ndoa iliyokuwa na miingiliano mingi kutoka kwa seneta Karen Nyamu ambaye ni babymama wa mumewe, Samidoh.

Nderitu alisema kuwa ndoa yake ilikuwa imedumu kwa miaka 15 lakini akasisitiza kwamba hakuwa tayari kuendelea kuwalea wanawe katika ndoa yenye wake Zaidi ya mmoja.

Miezi michache baadae, aliweka wazi kwamba amefanikiwa kuwaingiza wanawe katika mfumo wa masomo wa Marekani, ishara iliyoonesha kwamab hakuwa tayari kurudi nchini tena.

Licha ya kudai kwamba hangeweza kumruhusu Samidoh kuwaona wanawe, miezi michache iliyopita wakati wa ziara yake Marekani, Samidoh alionekana akijumuika na wanawe kwa furaha na bashasha.