Skales, msanii wa Afrobeats alia kuwa mpweke na kukosa furaha licha ya kuwa na pesa nyingi

“Mimi ni mwanamume mpweke ambaye anahofia maisha yangu kila siku. Sina mtu kabisa, mapenzi ya kweli ambayo niliwahi kuhisi ni yale kutoka kwa mamangu, sasa ameshafariki, duh!” alisema

Muhtasari

• Mwimbaji-mtunzi wa wimbo alisema kuwa hana mtu, isipokuwa binti yake, ambaye alizaa na mkewe waliyeachana naye.

Skales alia upweke
Skales alia upweke
Image: Instagram

Mwimbaji wa Nigeria Skales ameelezea hofu yake na wasiwasi wake katika maneno marefu ya hivi majuzi huku akilalamika kuhusu misukosuko anayopitia.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii aliandika kuhusu jinsi alivyokuwa mpweke na kwamba hakuna mtu anayejali maslahi yake moyoni.

Mwimbaji-mtunzi wa wimbo alisema kuwa hana mtu, isipokuwa binti yake, ambaye alizaa na mkewe waliyeachana naye.

Kando na upweke wa kimapenzi, msanii huyo pia alimkumbuka marehemu mama yake akisema kwamba yeye ndiye mwanamke wa pekee aliyekuwa anamsikiliza na kumuelewa, ka kwamba kifo chake kinadhihirika kuwa pigo katika maisha yake.

"Mapenzi ni mzaha katika kizazi hiki. Mapenzi ni ujinga. Bora upende kimkakati, mapenzi ya kweli ambayo niliwahi kuhisi ni yale kutoka kwa mamangu, sasa ameshafariki, duh!” alisema.

Alisema zaidi kwamba anahofia maisha yake, yuko mpweke sana, na hakuna mtu anayependa zaidi moyoni mwake

“Mimi ni mwanamume mpweke ambaye anahofia maisha yangu kila siku. Sina mtu kabisa. Inatisha… nilimfahamu Mungu… lakini upendo ni upuuzi. Amini ujinga huo kwa hatari yako mwenyewe."

Katika slaidi nyingine, aliandika hivi: “Hii ndiyo mvunjiko zaidi kama mwanaume ambaye nimewahi kuhisi. Nimemkumbuka mama yangu kwa sababu ningekuwa kwenye simu naye sasa hivi.”

“Sikiliza mjinga. Nilipata pesa… Lakini niko mpweke ASF… Namkumbuka mama yangu. Sina mtu yeyote wa familia, sio shangazi wala mjomba, sio baba wala mama, sina hata mpenzi. Namshikilia tu Mungu, ni jambo la kutisha sana, kama wewe una familia ni jambo la kumshukuru Mungu kila wakati,” aliongeza.