'Lazima nioe wake zaidi ya wawili,' Mbunge Salasya

Salasya ambaye amekuwa gumzo kwa sababu ya maoni yake tata na kashfa nyingi mtandaoni, alidai kuwa ana pesa za kuwatunza wake zake.

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram , Salasya alizua gumzo kati ya wanamitandao baada ya kusema kwamba anafikiria kuoa wake zaidi ya wawili.
MBUNGE PETER SALASYA
Image: HISANI

Mbunge mwenye utata wa Mumias Mashariki Peter Salasya ameapa kuoa wanawake wengi akisema ana pesa za kuwatunza.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram , Salasya alizua gumzo kati ya wanamitandao baada ya kusema kwamba anafikiria kuoa wake zaidi ya wawili.

Anadai kuwa hali ya hewa ya sasa ya baridi ni kubwa na imemfanya aanze kufikiria kupata mwanamke mmoja huu mwaka na mwingine mwaka ujao.

"Hii baridi inaanza kunilazimisha kuanza kufikiria kupata mwanamke mmoja mwaka huu alafu mwingine mwaka ujao." Salasya aliandika.

Salasya ambaye amekuwa gumzo kwa sababu ya maoni yake tata na kashfa nyingi mtandaoni, alidai kuwa ana pesa za kuwatunza wake zake.

"Lazima nioe zaidi ya wake wawili pesa ya kuwalinda iko kidogo ya kuwa kudumisha." Mbunge huyo alihitimisha.

Chapisho lake linakuja baada ya wiki moja tu baada ya aliyekuwa Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kujulikana kwa madai ya kumtambulisha mke wake wa tatu Mary Biketi kwa Umma na kuthibitisha kwamba ana wake wengi.

Seneta wa Kakamega Bony Khalwale amekiri hadharani kuwa na wake wengi.