Sijawahi kuumizwa moyo na mwanamke yeyote maishani mwangu - Jay Melody

Melody alisema amefanya mambo kadhaa ya kuvunja moyo kwa wanawake lakini hajawahi kuyapitia yeye mwenyewe.

Muhtasari

•Melody alisema amefanya mambo kadhaa ya kuvunja moyo kwa wanawake lakini hajawahi kuyapitia yeye mwenyewe.

•Sijawahi kuumizwa na Mapenzi maishani labda mimi ndio nimumize Mtu.

Jay Melody.
Jay Melody.
Image: Instagram

Melody alisema amefanya mambo kadhaa ya kuvunja moyo kwa wanawake lakini hajawahi kuyapitia yeye mwenyewe

Mwimbaji kutoka Tanzania Jay Melody anayefahamika kwa kuachia nyimbo kibao za mapenzi amefichua kuwa kamwe katika maisha yake hajawahi kuumia moyo kutokana na mapenzi.

Melody alisema amefanya mambo kadhaa ya kuvunja moyo kwa wanawake lakini hajawahi kuyapitia yeye mwenyewe.

“Sijawahi kuumizwa na Mapenzi maishani labda mimi ndio nimumize Mtu.” Alisema 

Alitoa mfano wa mwanamke ambaye alikataa wanaume wengi lakini akamchangua yeye lakini baadae alimkataa.

Jambo kubwa ambalo siwezi kulisahau ni kumkataa mrembo aliyetongozwa na wanaume 16 lakini hakuwataka, alinichagua nikakataa.”

Melody alithibitisha kuwa anachumbiana  “Napenda maisha ya hali ya chini, sipendi kumpost mpenzi wangu, nikifanya hivyo ina maana nafunguka mambo mengi, watu wenye pesa wataanza kumpiga, sipendi maisha yangu. sana kwenye mitandao ya kijamii hadi nashindwa kuiishi."