Andrew Kibe azungumza kuhusu uhusiano na mke wake wa zamani

"Najua pengine ananingoja niwe tajiri kuliko nilivyo sasa hivi" - Andrew Kibe kuhusu uhusiano wake na mke wake wa zamani.

Muhtasari

•"Najua pengine ananingoja niwe tajiri kuliko nilivyo sasa hivi."

Andrew Kibe/Instagram
Andrew Kibe/Instagram

Muunda maudhui Andrew Kibe amekiri tabia yake ya zamani, na kufichua kwamba amekuwa 'simp’ siku zote.

Katika mazungumzo ya hivi majuzi, Kibe aliangazia matukio ambapo matendo yake yaliakisi tabia hii, na kumpelekea kutathmini upya mtindo wake wa maisha.

Alifichua kuwa hawakuwahi kuachana rasmi na alikisia kuwa mke wake wa zamani huenda anamngoja apate  mali zaidi  kabla ya kuchukua hatua zozote za kisheria.

"Najua pengine ananingoja niwe tajiri kuliko nilivyo sasa hivi," Kibe alisema.

Licha ya kutokuwa na uhakika kuhusiana na hali ya uhusiano wao, Kibe alionyesha kutopenda kuoa tena.

Kibe alifichua katika mahojiano yaliyopita kwamba alihisi kushinikizwa na wachungaji wake kuoa. Pia alieleza kuwa kabla ya ndoa yake, alitakiwa kufunga siku tatu.

Kibe alisimulia kuingizwa kanisani na kufunga ndoa ndani ya muongo mmoja baada ya kujiunga.

Hata hivyo, ndoa yake iliisha, na alikiri wazi kuwa alihusika na wanawake wengi katika kipindi hicho.