Anerlisa Muigai asema rafiki zake ni waongo

Mazungumzo yaliyoenea yalikuwa kutoka kwenye kikundi chenye marafiki wa Anerlisa pekee.

Muhtasari

•Mazungumzo yaliyoenea  yalikuwa kutoka kwenye kikundi chenye marafiki wa Anerlisa pekee.

• Marafiki wa kweli ni kama nyota, huwaoni kila wakati lakini wapo kila wakati

Amerlisa Muigai
Amerlisa Muigai
Image: instagram

Mfanyabiashara Anerlisa Muigai amewaita 'rafiki' zake waongo baada ya kueneza mazungumzo ya faragha kutoka kwa kikundi cha WhatsApp.

Mazungumzo hayo yalikuwa ya Anerlisa kuomba pesa za kumnusuru anayedaiwa kuwa mchumba wake Josiah Kariuki.

Kariuki alishtakiwa Mei 6 katika Mahakama ya Kupambana na Ufisadi ya Milimani kwa madai ya kutengeneza, kusambaza na kuuza mbolea duni.

Anerlisa alielezea masikitiko yake akisema marafiki bandia ni kama kivuli.

"Ulipofikiri una marafiki wa kweli basi boom. Kesho unaweza kuwa wewe. Angalau najua siwezi kutegemea kila mtu na ni sawa. Na ndio tuliweza kutoka bila msaada yako.  #Mungu Kwanza," sehemu ya chapisho lake ikizungumzia suala hilo ilisomeka.

Aliweka chapisho ambalo lilionya watu juu ya jinsi ya kutofautisha kati ya marafiki bandia na wa kweli.

"Marafiki wa uongo ni kama vivuli: huwa karibu nawe nyakati zako zenye kung'aa sana lakini hakuna mahali unapoweza kuonekana katika saa yako ya giza kabisa. Marafiki wa kweli ni kama nyota, huwaoni kila wakati lakini wapo kila wakati," nukuu hiyo ilisoma.

Josiah ambaye alihusishwa na usambazaji wa mbolea ghushi alishtakiwa kwa makosa 7 ambayo ni pamoja na kula njama ya ulaghai, kubadilisha hati za uwongo, pamoja na kutumia alama ya kusanifisha kwa bidhaa ambayo haizingatii viwango vya Kenya na sheria zingine.