“Ndoto yangu ni kuwa baba wa mabinti 3!” – Eric Omondi

“Mtoto wa kike ni wa baba, inakuja na hisia Fulani nzuri kwani Mungu alijibu maombi yangu. Mimi tangu utotoni nilikuwa nimeomba nipate watoto wa kike watatu. Nishampata mmoja, bado wawili,” Omondi alisema.

Muhtasari

• Kuhusu kufunga harusi kabisa na kumfanya Lynne kuwa mkewe rasmi, Omondi alisema;

 
• “Kuhusu ndoa, sisi ni watu wa surprise. Lolote linaweza kutokea wakati wowote.”

Eric Omondi
Eric Omondi
Image: Facebook

Mchekeshaji aliyegeuka na kuwa mwanaharakati Eric Omondi amezungumzia fahari ya kuwa baba kwa mtoto wa kike.

Akizungumza na blogu ya Rick Media baada ya kutua nchini Tanzania, Omondi alisema kuwa anajihisi angalau yuko katika mkondo salama kufanikisha ndoto yake.

Mwanaharakati huyo mwenye shughuli nyingi za kiharakati kando na familia alisema kuwa tangu utotoni, ndoto yake imekuwa kuitwa baba wa mabinti watatu, na kusema kwamba kumpata binti wa kwanza, Kyla ilikuwa kama mwanzo wa majibu kwa ndoto zake za utotoni.

“Mtoto wa kike ni wa baba, inakuja na hisia Fulani nzuri kwani Mungu alijibu maombi yangu. Mimi tangu utotoni nilikuwa nimeomba nipate watoto wa kike watatu. Nishampata mmoja, bado wawili,” Omondi alisema.

Omondi pia alizungumzia ukuaji wa bintiye Kyla na kusema kwamba ameshakua kwa kasi ya ajabu na ivyo itampa fursa yeye na mpenziwe Lynne kutathmini kupata watoto wengine wawili – mabinti – ili kutimiza ndoto yake ya utotoni.

“Kyla kashakua kwa haraka sana, yani unalala, unafumba na kufumbua, kakua,” alisema.

Kuhusu kufunga harusi kabisa na kumfanya Lynne kuwa mkewe rasmi, Omondi alisema;

“Kuhusu ndoa, sisi ni watu wa surprise. Lolote linaweza kutokea wakati wowote.”