Amber Ray afichulia mashabiki wake upasuaji anaotarajia hivi karibuni

"Unajua nimewanyonyesha watoto wote wawili na wanaume wazima kwa hivyo kwa kweli hawako katika nafasi nzuri ninayotaka wawe.

Muhtasari
  • Mwanasosholaiti huyo ambaye kwa sasa amechumbiwa na mfanyabiashara Kennedy Rapudo aliendelea kuongeza;

Mtayarishaji wa maudhui ya kidijitali, mtangazaji wa klabu na mshawishi wa chapa Faith Makau, anayejulikana sana mitandaoni kama  Amber Ray amewafichulia mashabiki wake upasuaji ambao anaotarajia hivi karibuni.

Akiwa kwenye mahojiano, mama huyo wa watoto 2, ambaye anapenda kujiita 'bibi yatajari' alifunguka kuhusu nia yake ya kufanyiwa mastopexy inayojulikana pia kama kunyanyua matiti.

"Matiti yangu, nataka zisimame,alianza Amber Ray wakati akijibu swali la, ikiwa ana ndoto za kufanya upasuaji wowote wa plastiki.

Mwanasosholaiti huyo ambaye kwa sasa amechumbiwa na mfanyabiashara Kennedy Rapudo aliendelea kuongeza;

"Unajua nimewanyonyesha watoto wote wawili na wanaume wazima kwa hivyo kwa kweli hawako katika nafasi nzuri ninayotaka wawe. Kwa hivyo katika siku zijazo, ndio, kwa kweli ... natumai hivi karibuni sijali.

Oohh Mungu wangu, sijali, ningependa kupata moja,"

Kugusia ikiwa kupata upasuaji kulimaanisha kwamba ameamua kufunga sura ya watoto, mtayarishaji wa maudhui ya kidijitali alisema hapana. Anapenda kuwa mama na bado anatumai kuwa amebarikiwa kuendelea kukuza familia yake.

"Unaweza kufanya kazi ya boob na bado ukawa na watoto wengi zaidi. Kwa sababu bado nataka watoto zaidi, labda ninafikiria watoto 2 au 3 lakini yote inategemea pesa kwa sababu nataka kuwapa watoto wangu bora zaidi maishani," sosholaiti alisema kwa uwazi.

"Kwa hivyo ninafikiria watoto 4 au 5 wote pamoja," Amber aliongeza.