Burna Boy aripotiwa kumnunulia mamake Benz mpya kama zawadi ya siku ya kina mama

Itakumbukwa kwamba Burna Boy amewahi kiri mara si moja kwamba yeye ni mtoto wa mama na hata kufichua ukaribu wake na mamake mpaka kufikia hatua ya kumteua kama meneja wa kazi zake za Sanaa.

Muhtasari

• Akiwa kwenye moja kwa moja, Burna Boy alifichua kwamba alirudi nyumbani kusherehekea Siku ya Akina Mama na mama yake na kumpa zawadi ya usafari mpya.

• Mwaka huu, siku ya akina mama duniani iliadhimishwa Jumapili ya Mei, tarehe 12.

Image: Hisani

Mwimbaji nyota wa kimataifa wa Nigeria, Damini Ogulu, almaarufu Burna Boy, amekuwa gumzo la mitandao ya kijamii, safari kwa lengo zuri baada ya video kusambaa akidaiwa kumnunulia mamake zawadi ya gari jipya aina ya Mercedes Benz kuadhimisha siku ya kina mama duniani.

Klipu ya Burna Boy na mama yake wakipiga picha mbele ya gari hilo la kifahari ilisambaa mitandaoni na kuvutia pongezi na hongera kutoka kwa mashabiki kwa kuonesha jinsi anavyomjali na kumdhamini mamake.

Itakumbukwa kwamba Burna Boy amewahi kiri mara si moja kwamba yeye ni mtoto wa mama na hata kufichua ukaribu wake na mamake mpaka kufikia hatua ya kumteua kama meneja wa kazi zake za Sanaa.

Katika kipande hicho kinachovuma, mamake Burna Boy alionekana akizungumza na nyota huyo wa Afro-fusion huku akimshukuru kwa kumkabidhi zawadi hiyo ya kifahari kwa ajili ya Siku ya Akina Mama.

Saa kadhaa baada ya kumpa mama yake zawadi ya Mercedes Benz Maybach SUV, mwimbaji huyo aliendelea na IG moja kwa moja.

Akiwa kwenye moja kwa moja, Burna Boy alifichua kwamba alirudi nyumbani kusherehekea Siku ya Akina Mama na mama yake na kumpa zawadi ya usafari mpya.

Mwaka huu, siku ya akina mama duniani iliadhimishwa Jumapili ya Mei, tarehe 12.

Siku hii spesheli kwa kina mama inaadhimishwa kila Jumapili ya pili ya mwezi Mei kila mwaka.