Kamene Goro asimulia vile DJ Bonez alimtunza wakati hakuweza kutembea

Sijawai kulalamika,Katika miezi hiyo miwili, Kamene aeleza jinsi mumewe alisimama naye na kumtunza kwa upendo.

Muhtasari

•Mtangazaji wa redio Kamene Goro alielezea mateso yake ya maumivu ya goti ambayo yalimfanya afanyiwe upasuaji mara kadhaa.

•Sijawai kulalamika,Katika miezi hiyo miwili, Kamene aeleza jinsi mumewe alisimama naye na kumtunza kwa upendo.

kamene goro, dj bonez
kamene goro, dj bonez

Kamene Goro amefunguka kuhusu kipindi kigumu kufuatia jeraha la goti ambalo lilimfanya ashindwe kutembea kwa takriban miezi miwili.

Kamene alishiriki maelezo ya masaibu yake kwenye ngoti ambayo yalisababisha upasuaji mara nyingi, upasuaji wa mwisho ukifanyika Januari.

Kamene alisema  aliwekwa chuma kwenye mguu wake, na kumfanya ashindwe kutembea kwa takriban miezi miwili.

Alieleza vile DJ Bonez alisimama na yeye na kumtunza kwa miezi miwili ambayo angeweza kutembea kutokana na upasuaji huo.

"Miaka mitano iliyopita ndo  nilipata kitu inaitwa meniscus tear. Nikafanya upasuaji wa kwanza, halafu wiki nne baadae nikafanya upasuaji wa pili kwa sababu ulichanika tena. Kisha nikakaa kiasi cha miaka kadhaa halafu mwaka jana ikarejea tena. Sijawahi kuhisi maumivu kama hayo maishani mwangu, kwa hiyo, mwezi wa Januari, nilifanyiwa upasuaji tena nilianza kujifundisha jinsi ya kutembea siku ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwangu,” alisimulia.

Wakati huu wa majaribu, mumewe, DJ Bonez, alisimama na kumtunza kwa upendo. Kamene alitoa shukrani kwa kujitolea kwa Bonez, akibainisha kuwa hakuwahi kulalamika hata siku moja.

 "Unajua anakusafisha, alikuwepo kila siku bila kukosa....'babe leo tunakula hii, dawa ndo hizi, vipi uko Je, uko sawa naweza kukufanyia hivi?' Yeye ndo alikuwa hapo kila siku," alisema.

 “Familia yangu iliniunga mkono sana, wakati wa kupona ulikuwa mungumu hata kulala kwa sababu nilikuwa nalala na hiyo chuma. Kwa hivyo huwezi kulala. "aliongeza