Siku chache zilizopita imani yangu imejaribiwa:Size 8

Hakika nimeuona mkono wa Mungu,” Size 8 aliandika.

Muhtasari

• Size 8 alitumia hadithi ya Shadraka, Meshaki na Abednego kutoa ushuhuda wake.

•"Tunaweza pia kupitia majaribu au mtihani lakini kumbuka  yanaweza kujitokeza kwa njia nyingi na ni mtihani wa imani yetu,"aliongeza

size 8
Image: instagram

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Size 8 amefunguka kuhusu kupitia siku kadhaa ngumu huku akiwashukuru watu wake wa karibu kwa kuwa karibu naye wakati wa majaribu.

Alitumia  mtandao yake ya kijamii kuangazia jinsi imani yake ilivyojaribiwa na pia kuwatia moyo watu  ambao huenda wanapitia wakati mgumu pia.

"Siku  chache zilizopita imani yangu imekuwa kwenye mtihani. Shukrani kwa wote ambao wamesimama pamoja nami na familia yangu katika maombi.

Hakika nimeuona mkono wa Mungu,” Size 8 aliandika.

Aliendelea kunukuu kutoka katika Biblia kisa cha Shadraka, Meshaki na Abednego ambao wanajulikana kuchomwa na moto wakiwa hai lakini hawakuchomeka na jinsi anavyofarijiwa na ukweli kwamba wale 3 walitembea katika tanuru na wakatoka hai. kwa sababu Mungu alikuwa pamoja nao.

"Tunaweza pia kupitia majaribu au mtihani lakini kumbuka  yanaweza kujitokeza kwa njia nyingi na ni mtihani wa imani yetu,"aliongeza.

Kufikia mwisho wa chapisho lake katika mtandao wake ya instagram, Size 8 aliendelea kutoa neno la kutia moyo kwa watu  ambao wanaweza kuwa wakipitia majaribu akiwakumbusha kuwa ameshuhudia kuwa mtu hayuko peke yake.

Pia aliwahimiza kushikilia mema ambayo yametokea katika maisha wakati wa giza au majaribu.

"Shikilia imani yako kwa maana siku zote kuna mtu wa nne kwenye majaribu, hatuko peke yetu. Na usisahau mazuri ambayo Mungu tayari amefanya katika maisha yako," mwisho wa chapisho lake ilisomeka.

 Akinukuu chapisho hilo, alifafanua baadhi ya njia ambazo anahisi majaribu yanaweza kujidhihirisha katika maisha ya kisasa akinukuu mambo kama vile,"ugonjwa, kupoteza mpendwa, mafuriko, matatizo ya ndoa na kupoteza mali, ukosefu wa karo na chakula.”