Jude Magambo afichua kwa nini anatamani kukutana na Brian Chira ndotoni mara kwa mara

"Wakati mwingine huwa naketi tu kwa nyumba najisemea ‘si akuje tu hapa kwa kitanda’. Siwezi kimbia,” Magambo alisema.

Muhtasari

• Manzi wa Meru alidai kuwa Chira anaishi katika fikira zake. Alisema endapo Chira angetokea kwa sasa, atamkumbatia kwa nguvu.

Manzi wa Meru na tatoo ya Brian Chira.
Manzi wa Meru na tatoo ya Brian Chira.
Image: Screengra// KOM (YouTube)

 Jude Magambo almaarufu Manzi Wa Meru amefichua kwamba anakosa uwepo wa aliyekuwa rafiki yake, Brian Chira katika mzunguko wa maisha yake ya kila siku.

Akizungumza katika mahojiano hivi majuzi na blogu moja, Magambo alisema kwamba anatamani Chira awe akimtokea kama mzimu kwenye nyumba yake, akisema kwamba haogopi wala hatatoroka kuona Chira kama mzimu.

Manzi wa Meru alidai kuwa Chira anaishi katika fikira zake. Alisema endapo Chira angetokea kwa sasa, atamkumbatia kwa nguvu.

“Amekufa lakini Chira anaishi ndani yangu ambayo hata akitokea hapa [kama mzimu] nitaenda na kumkumbatia kwa nguvu sana. Wakati mwingine huwa naketi tu kwa nyumba najisemea ‘si akuje tu hapa kwa kitanda’. Siwezi kimbia,” Magambo alisema.

Alifichua kwamba anapanga kwenda kuzuru kaburi lake katika wiki ijayo. Alitaja lengo la yeye kutembelea makaburi hayo ni kumsalimia marehemu Brian Chira.

"Nitaenda kumwambia na kuzungumza naye kwa dakika 5 na kumwambia kuwa ninamkumbuka sana. Ningetamani aje kwenye ndoto zangu. Tangu azikwe sijawahi kumuota. Nataka kuota naye,” alisema na kuongeza kuwa watu walimdharau kwa kuunganishwa na wafu baada ya kuchora tattoo ya uso wa Chira.

Manzi wa Meru alikutana na Chira kwenye TikTok na wawili hao walitangamana kwa kuwa walikuwa wameanzisha urafiki mkubwa. Waliunda kumbukumbu zisizosahaulika ambazo bado zinamsumbua hadi leo.

Chira alifariki mapema mwezi Machi katika ajali ya barabarani, kifo ambacho kimekuwa kikizua simulizi zenye mitazamo na dhana tofauti tofauti.