logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Kitu najutia katika maisha yangu ni kusaidia mtu mwenye hakuhitaji usaidizi” – Baba Talisha

Ifahamike kwamba Baba Talisha katika siku za hivi karibuni amekuwa katika mzozo mkali na bibiye Brian Chira.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 May 2024 - 06:46

Muhtasari


  • • Ifahamike kwamba Baba Talisha katika siku za hivi karibuni amekuwa katika mzozo mkali na bibiye Brian Chira.

TikToker Faustine Lipuku Lukale maarufu kama Baba Talisha amefunguka kwamba kwa sasa kitu ambacho anakijutia pakubwa katika maisha yake ni kunyoosha mkono wa usaidizi kwa mtu ambaye hakuwa anastahili kupatiwa usaidizi.

Akizungumza na waandishi wa habari za burudani katika hafla ya uzinduzi wa filamu ya Monkey Business yake msani King Kaka katika ukumbi wa Two Rivers mwishoni mwa juma, Baba Talisha alisema kwamba amejifunza mengi na kikubwa ni kujinyamazia kwa sababu aligundua akiendelea kuzungumza Zaidi ndivyo anavyozidi kuvutia mizozo Zaidi.

“Kitu ambacho nimejifunza ni kwamba muda wote usisahau unachofanya, na kuwa wewe. Mimi nitaendelea kufanya kilicho sahihi, kwa sababu kuna mtu anaangaia kutoka mahali katika haya maisha. Nimegundua kwamba kila mtu unapozungumza ndivyo unavyozua mzozo Zaidi, na mimi huwa sipendi hizo drama,” alisema.

“Kumekuwa na maneno mengi lakini mimi nimeamua kuwa katika mstari wangu tu, sitaki mambo mingi. Na kitu kikubwa ambacho ninajutia ni kusaidia mtu mwenye hakuhitaji usaidizi, hayo ndio majuto ambayo niko nayo,” aliongeza.

Ifahamike kwamba Baba Talisha katika siku za hivi karibuni amekuwa katika mzozo mkali na bibiye Brian Chira katika kile kinachotajwa kuwa ni uwajibishaji wa jinsi hela zilizochangishwa kwa ajili ya mazishi ya TikToker huyo zilivyotumika.

 

Baba Talisha alichukua jukumu kuu la kuwaasa watumizi wa mtandao wa TikTok kuchangisha hela kwa ajili ya mazishi ya Brian Chira ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu.

Watu walichangisha Zaidi ya milioni 8 ambazo Baba Talisha aliratibu kwa ajili ya mipangilio mbalimbali na kusalia na milioni 7.2 kwenye akaunti ambazo alisema wameafikiana na bibiye Chira kuzipangia mambo mengine kumfaidisha yeye.

Hata hivyo, bibi huyo hivi majuzi alikwenda kwenye mitandao ya kijamii akifoka kwa hasira kwamba hajui jinsi pesa hizo zinavyotumika na kumburuta Baba Talisha akitaka kumwajibisha kwa kila senti na hata kutaka salio hilo kukabidhiwa kwake mara moja.

Hili liliwagawanya wanamitandao, baadhi wakimsuta bibi huyo kwa kukosa fadhila kwa Baba Talisha huku wengine wakisema kwamba alikuwa na kila haki ya kuulizia ziliko pesa zilizochangishwa kwka ajili ya mazishi ya mjukuu wake.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved