“Mbona ndoa za siku hizi hazidumu kama za enzi za mababu zetu?” Brown Mauzo ahoji

Mauzo alisema kuwa uhusiano alio nao wa kimapenzi kwa sasa ndilo jaribio lake la mwisho, na endapo utaenda mrama basi atatundika daluga zake na kuondoka katika uwanja wa kusumbua moyo wake kutafuta mapenzi.

Muhtasari

• “Kama uhusiano nilioko ndani utakosa kufanya kazi, basi nitakuwa nimemalizana na mambo ya mahusiano,” Mauzo aliongeza.

• Baada ya kuachana na Vera Sidika mwezi Septemba mwaka jana, baba huyo wa watoto wawili alichukua muda mfupi kujisitiri kwa kupata mpenzi mwingine kwa jina Kabinga Jr.

Brown Mauzo na mpenzi mpya.
Brown Mauzo na mpenzi mpya.
Image: Instagram

Msanii Brown Mauzo amezua mjadala mkali kupitia insta story zake akihoji kwa nini ndoa nyingi za kizazi cha sasa huwa hazidumu kama za vizazi vya watu wa zamani.

Baba huyo wa watoto wawili na mwanasosholaiti Vera Sidika anahoji kwamba ndoa za kisasi cha sasa zinavunjika na kusambaratika kwa kasi ya ajabu ikilinganishwa na ndoa za enzi za mababu.

“Mbona ndoa hazidumu kama zile za enzi za mababu zetu?” Mauzo aliuliza akisema kuwa ni mjadala wazi ambao yeyote ako na ruhusa ya kuchangia.

Kwa upande wake, Mauzo alisema kuwa uhusiano alio nao wa kimapenzi kwa sasa ndilo jaribio lake la mwisho, na endapo utaenda mrama basi atatundika daluga zake na kuondoka katika uwanja wa kusumbua moyo wake kutafuta mapenzi tena.

“Kama uhusiano nilioko ndani utakosa kufanya kazi, basi nitakuwa nimemalizana na mambo ya mahusiano,” Mauzo aliongeza.

Baada ya kuachana na Vera Sidika mwezi Septemba mwaka jana, baba huyo wa watoto wawili alichukua muda mfupi kujisitiri kwa kupata mpenzi mwingine kwa jina Kabinga Jr.

Waliachana na Sidika baada ya uchumba wa miaka 3 uliozalisha watoto wawili, Asia Brown na Ice Brown.

Kkwa mujibu wa taarifa zao, wawili hao hawakukosana bali ni mapenzi yaliisha na kuchokana, na hivyo wakaona ni akheri kila mmoja akajitenga na kujishughulisha na hamsini za kwake.

Hata hivyo, katika suala la malezi ya wanao, Mauzo na Sidika wamekuwa wakishirikiana kikamilifu, mara kwa mara watoto wakionekana na wazazi kutoka pande zote mbili.