logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Anapenda bedroom!” Ringtone aeleza sababu ya kukataa ombi la Justina Syokau kimapenzi

Hivi vitu vya dunia mnaangalia sio vyenye mimi ninaangalia - Ringtone.

image
na Davis Ojiambo

Burudani22 May 2024 - 13:12

Muhtasari


  • • Katika mahojiano ya hivi majuzi, Ringtone alifunguka kwa uwazi sababu zilizomfanya kupiga chini ombi la Justina Syokau kutaka wawe wapenzi na kueneza injili kwa pamoja kama familia.
Wasanii wa injili Ringtone na Justina Syokau

Msanii anayejiita mwenyekiti wa tasnia ya injili, Ringtone Apoko kwa mara nyingine amerejelea utani wake na Justina Syokau kuhusu kupendana.

Ikumbukwe kwa Zaidi ya miaka miwili iliyopita, Justina Syokau alikiri katika mahojiano mbalimbali kwamba alikuwa anatamani sana kuolewa na mwenyekiti wao katika injili, Ringtone Apoko.

Hata hivyo, Ringtone, ambaye hajaoa licha ya kufanikiwa kimuziki kwa muda mrefu alionekana kucheza mchezo wa paka na panya kwa hisia za Syokau, akikwepa kuzungumzia iwapo angekubali ombi lake au la.

Katika mahojiano ya hivi majuzi, Ringtone alifunguka kwa uwazi sababu zilizomfanya kupiga chini ombi la Justina Syokau kutaka wawe wapenzi na kueneza injili kwa pamoja kama familia.

Kwa mujibu wa Ringtone, yeye anatafuta mwanamke ambaye atatumikia muda wake mwingi katika kumsifu Mungu lakini utafiti wake ulimuonyesha kwamba Justina anapenda kutumia muda mwingi katika chumba cha kulala.

“Hivi vitu vya dunia mnaangalia sio vyenye mimi ninaangalia. Kitu cha kwanza mimi ninaangalia msichana ambaye anapenda Mungu, anaweza omba kwa saa 7 mfululizo kwa siku. Mwenye anafahamu kwamba Mungu alituumba tuende tujaze dunia na anaheshimu hiyo katika Biblia. Kwa kifupi mimi nataka msichana mwenye ako na ari na mambo kuhusu Mungu,” Ringtone alisema.

“Niliangalia Justina anasema eti anataka nimuoe, ikabidi nifanye uchunguzi wangu na nikagundua kwamba anapenda kushiriki mapenzi sana. Anapenda kushinda bedroom. Mimi naye yule msichana nataka sitaki tushinde bedroom, nataka tushinde tukihubiri,” aliongeza.

Ringtone alisisitiza kwamba kuna baadhi ya sifa na vigezo vingi tu ambavyo ataviagalia katika mwanamke wa kumuoa, akisema kwamba hatojali kama ni wa mjini au kijijini ilmradi atomize vigezo vyote.

“Niko na qualities nimeset za msichana. Msichana yeyote mwenye ana qualify, awe wa kijijini au mjini, mfupi au mrefu, mweusi au mweupe, mwenye umbo zuri nene au bila umbo nene, wote wamehitimu kwangu. Haya mambo ya kidunia mnaangalia sio yenye mimi ninaangalia,” alisisitiza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved