Commentator 254:Mpenzi wangu huniosha miguu kila siku

Muunda maudhui huyo amesema kuwa mpenzi wake Moureen Ngigi huosha miguu yake kila siku.

Muhtasari

•Commentator 254 aelezea mapenzi anayopewa na mpenzi wake

•Wawili hao wako na mtoto mmoja kijana mwenye umri wa mwezi moja

Commentator254 na mpenziwe Moureen. Picha;Instagram
Commentator254 na mpenziwe Moureen. Picha;Instagram

Muunda maudhui wa Kenya, Commentator 254, ameelezea  ubora wa kuchumbiana na mwanamke mwafrika.

Katika video iliyosambazwa kwenye mtandao wa Instagram, Commentator alisema kuwa baada ya siku nyingi kazini, huwa anatazamia kwenda nyumbani kwa mpenzi wake Moureen Ngigi kwa sababu ya mapenzi anayompa.

Wawili hao walishiriki video ya jinsi jioni yao hukuwa  baada ya kufika nyumbani. Kwenye video Moureen anaonekana akimsalimia mlangoni, akichukua begi la ununuzi na kuvua koti lake. Kisha anaendelea kuchota beseni la maji ya joto ambalo anatumia kuosha miguu yake.

Moureen anaonekana akipiga magoti sakafuni huku akiosha miguu ya mtu wake na kuendelea kuikausha huku uso wake  ukionyesha tabasamu na baadaye  kumletea viburudisho.

Mashabiki hata hivyo wametoa maoni tofauti huku baadhi wakidai kuwa ni video iliyoandikwa inayolenga kutoa mwonekano.Huku wengine wakisema ishara ndogo kama hizo hufanya ndoa ifaulu.

Katika mahojiano ya awali na Nicholas Kioko, alifichua  kuhusu kupatana na mpenzi wake, Moureen Ngigi, na jinsi alivyochukua nafasi yake.Commentator  alisema kuwa Moureen ndiye aliyewasiliana naye baada ya kufikisha watu laki moja wanaofuatilia YouTube yake, na hapo ndipo mazungumzo yao yalipoanza. Wanandoa hao kwa sasa wako na mtoto mmoja kijana mwenye  umri wa mwezi moja