Ezekiel mutua atishia kumpiga marufuku Kanyari kwenye tiktok na kumkamata

Matukio ya hivi majuzi yalionyesha Kanyari akikabidhiwa kondomu na mafuta aina ya arimisi kanisani hivo kuleta utata miongoni mwa wakenya

Muhtasari

•Ezekiel Mutua atishia kumpiga marufuku mchungaji mwenye utata,Kanyari,baada ya matukio ya kushangaza kwenye tiktok

Ezekiel Mutua
Ezekiel Mutua
Image: Facebook

Mchungaji Victor Kanyari amekuwa akiangaziwa hivi majuzi kwa uchezaji wake kwenye TikTok.

Wakenya wameachwa wakiwa wameburudika na kuchanganyikiwa na maudhui yake ya hivi majuzi. Kanyari anaonekana kutoogopa kuvuka mipaka, na hivyo kuzua maswali kuhusu ni umbali gani ataendelea na tabia yake.Matukio mawili ya majuzi yamezua mijadala mikali.

 Wakati wa ibada ya kanisani, 'Tiktoker' wa kike alimpa Kanyari zawadi ya kondomu, nguo za suruali, na mafuta aina ya Arimis. Ingawa wengine walisifu ujasiri wake, wengine waliona kuwa ni kukosa heshima katika mazingira ya kidini.

Aidha,Kanyari alizidisha mzozo kwa jaribio la ajabu la "kutoa pepo" kwa shoga maarufu aitwaye Mpenzi Chokuu. "Sala" ya Kanyari ilijumuisha matamshi ya kidini yaliyochanganywa na maneno ya kijeshi na ishara, huku Chokuu akipiga dansi. Kitendo hicho kilifurahishwa na wengine, wengine wakilaanina kusema ni kutoheshimu dini.

Vipindi hivi vinaonyesha ustadi wa Kanyari wa kuzua utata wakati huu,kwenye mtandao wa TikTok. Licha ya kukosolewa, Kanyari anadai motisha zake si kwa manufaa ya kibinafsi.

Katika video ya hivi majuzi, bosi wa MCSK Ezekiel Mutua anaeleza katika kongamano kwamba anatazamia kumpiga marufuku Kanyari kutoka jukwaani, akitaja kwamba amekuwa na utata mwingi. Anaongeza zaidi kwamba anastahili kukamatwa na kufungwa jela kwa mabishano hayo.

'Tutampiga marufuku Kanyari,na nitadai akamatwe na kufungwa...' Ezekiel alisema.