Ni uovu mtupu-Mchungaji T aeleza kwanini Kanyari sio mchungaji

Mchungaji T alisema inatosha na anachofanya Kanyari ni kinyume na Ukristo.

Muhtasari
  • Pia katika mahojiano , Pastor T alisema kuwa Kanyari ni mtayarishaji wa maudhui na watu hawapaswi kumwita mchungaji kwa sababu hajatimiza matakwa yoyote yanayohitajika kama kiongozi wa kidini.
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Pastor T

Mchungaji T Mwangi kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa  Facebook alimkashifu Mchungaji Kanyari, ambaye amekuwa akivuma kwa sababu zisizo sahihi katika wiki chache zilizopita.

Mchungaji T alisema inatosha na anachofanya Kanyari ni kinyume na Ukristo.

"Anayeitwa mtu wa Mungu kwenye TikTok lazima akomeshwe. Anachofanya hakihusiani na Ukristo, ni uovu mtupu,” alisema.

Pia katika mahojiano , Pastor T alisema kuwa Kanyari ni mtayarishaji wa maudhui na watu hawapaswi kumwita mchungaji kwa sababu hajatimiza matakwa yoyote yanayohitajika kama kiongozi wa kidini.

“Huyu kwanza huyo si pastor huyo ni content creator ukianglia maadili ya pastor na kile ambayo wachungaji wanafaa kufanya kila ofisi iko na specifications na demand na hakuna demand ame meet ,” alisema na kuongeza kuwa baadhi ya makanisa ni biashara tu sio madhabahu za Mungu.

Mchungaji T pia alisema kuwa serikali inaweza isiweze kudhibiti makanisa kama ya Kanyari, kwa sababu Kenya ni nchi isiyo ya kidini, akimaanisha kwamba kuna uhuru wa kusema na kuabudu hivyo basi serikali haiwezi iwaoneshe raia wake madhabahu gani wajiunge nayo au ni ipi wanayopaswa kujiunga nayo na ni ipi hawapaswi kujiunga.

Kanyari amekuwa akikashifiwa na kuonywa na baadhi ya wasanii,waunda maudhui kwa kuletewa kondomu na mafuta ya arimis kanisani na mmoja wa wafuasi wake kwenye tiktok.