Tileh Pacbro na mkewe Martina watangaza kuachana

Pacbro alieleza kuwa siku zote amekuwa mwaminifu kwa mwenzi wake kwani anathamini uaminifu

Muhtasari

•"Mimi na Martina tuliamua kuachana, hii ilitokea kitambo kutokana na tofauti kadhaa," amesema Pacbro.

•Miaka ambayo tumekaa pamoja imekuwa bora zaidi katika maisha yangu, nimeshuhudia furaha na ukuaji ambao siwezi kuhesabu.

Tileh na Martina
Image: Facebook

Mchezaji densi Tileh Pacbro na mkewe Martina Glez wametangaza kuachana kwa sababu ya tofauti zisizoweza kusuluhishwa.

"Sitakuwa na maneno sahihi ya kuandika haya, nimeitazama simu yangu kwa saa nyingi nikijaribu kutafuta maneno sahihi lakini hakuna kinachokuja. Mimi na Martina tuliamua kuachana, hii ilitokea kitambo kutokana na tofauti kadhaa," amesema Pacbro.

Baba huyo wa mtoto mmoja alisema kwamba miaka ambayo amekaa na Martina imekuwa bora zaidi na amepata ukuaji mkubwa. Aliongeza kuwa ingawa wameamua kwenda njia tofauti, daima watakuwa familia na washirika wa biashara.

"Miaka ambayo tumekaa pamoja imekuwa bora zaidi katika maisha yangu, nimeshuhudia furaha na ukuaji ambao siwezi kuhesabu. Safari yetu haijafika mwisho na haitawahi kwani tutabaki daima kuwa familia na kwa hilo tajajieni kutuona tukiwa pamoja, kwani sisi sio wazazi pekee bali pia washirika wa kibiashara."

Alieleza kuwa siku zote amekuwa mwaminifu kwa mwenzi wake kwani anathamini uaminifu

“Habari zimekuwa zikienea kutokana na ukimya wetu na kwa hilo naomba niweke wazi kuwa lolote ambalo baadhi ya mambo ambayo watu wanasema  sio mbali na ukweli na kila anayenifahamu mimi binafsi akiwemo Martina anafahamu jinsi ninavyothamini uaminifu na kila mara kwa kujigamba nilionyesha pete yangu wakati nilihitajika.

Nilikuwa na kila kitu nilichotaka kutoka kwake na sijawahi kuona sababu ya kutafuta mahali pengine. Tafadhali elewa kuwa maamuzi yoyote kati yetu kuchukua kuanzia sasa na kuendelea ni ya kibinafsi na haijaunganishwa kwa vyovyote vile na muungano wetu wa awali kwani utengano sio wa sasa kama chapisho hili limekuwa safari nzuri, kuna zaidi ya kuwa na furaha kuliko huzuni na hiyo itabaki hivyo milele,” Aliandika.