'Wivu tu ndio imewajaa...' Babushka awajibu wanaokosoa kazi zake za hisani

Babushka amewajibu wale wanaokosoa kazi yake wakidai kuwa anatafuta umaarufu.

Muhtasari

•Babushka amekuwa mstari wa mbele kutoa misaada huku baadhi wakisema anafanya hivyo ili kupata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii. 

BABUSHKA
BABUSHKA
Image: instagram

Mtayarishaji wa maudhui ya kidijitali Kennedy Matiso Rioba maarufu kama Babushka amejibu wale wanaomkosoa kuhusu kazi zake za uhisani.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Babushka ambaye amekuwa mstari wa mbele kutoa msaada kwa wahitaji alisema kwamba hataacha kazi yake ya uhisani kwa sababu ya kukosolewa baada ya kushutumiwa kwa kutumia kazi yake ya hisani kupata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii.

"Wivu tu ndio imewajaa, tutasonga mbele bila kujali," Mtayarishaji wa maudhui huyo alisema.

 Kennedy Matiso aliyeyusha mioyo ya mashabiki wake baada ya kufichua mipango yake ya kujenga daraja katika Kaunti ya Nairobi, Kasarani Machi, 2024 kupitia wakfu ya uhisani iliyopewa jina Babushka Foundation.

Huu ni mradi wake wa kwanza chini ya taasisi yake ya uhisani mbali na kazi yake ya hisani, Babushka anajulikana sana kwa kuburudisha watumiaji wa mtandao kupitia miondoko yake ya ngoma.