Amber Ray aeleza chanzo cha utajiri wa mpenzi wake Kennedy Rapudo

“Anafanya kazi kwa bidii, na anapata pesa nzuri inanifanya niwe vile niliko.” Amber Ray alisema.

Muhtasari

•“Anafanya kazi kwa bidii, na anapata pesa nzuri inanifanya niwe vile niliko.” Amber Ray alisema.

•Mimi ni mfanyabiashara na mwekezaji, na sitaki kuonekana huko nje napata pesa. Nilichagua kufanya watu wengi wasijue kwa sababu sisi kama Wakenya hatuungi mkono vitu za hapa kwetu.

Amber Ray
Image: HISANI

Mwanasosholati mashuhuri wa Kenya Faith Makau almaarufu Amber Ray akizungumza wakati wa mahojiano na Betty Kyallo alifunguka na kusema kuwa mumewe anafanya kazi kwa bidii na anatafuta pesa, ndio maana wana uwezo wa kufadhili sherehe za hali ya juu zinazohitaji mamilioni ya dola.

Hii ni baada ya maswali kuibuka baada ya wawili hao kuandaa sherehe iliyohudhuriwa na wasanii tajika nchini ya kusherehekea siku ya kuzaliwa wa mtoto wao.

“Anafanya kazi kwa bidii, na anapata pesa nzuri inanifanya niwe vile niliko.” Amber Ray alisema.

Kando na hayo, alisema yeye ni mfanyibiashara na muwekezaji ambaye anawekeza katika biashara nyingine nyingi na hamtegemei kabisa mumewe.

"Mimi ni mfanyabiashara na mwekezaji, na sitaki kuonekana huko nje napata pesa. Nilichagua kufanya watu wengi wasijue kwa sababu sisi kama Wakenya hatuungi mkono vitu za hapa kwetu, haswa linapokuja suala la biashara,”aliongezea.

Amber Ray pia alitoa ufafanuzi kwa nini hapendi kutangaza anachofanya mtandaoni, akisema ni kwa sababu kuna watu wanapenda kutoa mawazo mabaya kuhusiana na biashara za watu wengine na  aliamua kulinda amani yake kwa kutojihusisha na biashara anayomiliki na badala yake awape wengine.

“Maoni hayo hasi yanaendana sana hasa kwa biashara ndiyo maana kwangu, sitaki kamwe kujihusisha na biashara ninayofanya ni afadhali kumlipa mshawishi mwingine kutangaza biashara yangu au hata ninapoifanya nafanya hivyo kwa sababu si yangu.” Amber Ray alieleza.