KRG The Don atuma onyo kali kwa mwizi wa simu yake

ameahidi kutumia kiasi chochote cha pesa na kufanya lolote ili kumpata mwizi wa ambaye aliyeiba simu yake.

Muhtasari

•"Yaani Ukijua vile simu iko content huwezi kumudu kulala nayo. Eti biashara zangu zisimame juu ya mtu wa Boda Boda.Nitatumia hadi Ksh milioni 1 kurejesha iPhone yang,"

•“Mwiki sio mbali kwa serikali, tutakukamata kama kuku jua tu siku zako zinahesabika.Katika ujirani wetu, hii haitaendelea lazima uwe mfano." KRG aliandika.

KRG
KRG
Image: FACEBOOK

Msanii wa dancehall KRG The Don ameahidi kutumia kiasi chochote cha pesa na kufanya lolote ili kumpata mwizi wa ambaye aliyeiba simu yake.

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram, KRG alisema kuwa atafanya chochote kinachohitajika ili kurejesha simu yake, akikiri kwamba atatumia Ksh milioni 1 kufanya hivyo.

“Yaani Ukijua vile simu iko content huwezi kumudu kulala nayo. Eti biashara zangu zisimame juu ya mtu wa Boda Boda. Nitatumia hadi Ksh milioni 1 kurejesha iPhone yangu. Kesho nitaamka 5am nakutafuta na DCI kama ni Harusi tunaenda.” KRG aliandika.

Krg The Don alisema kuwa simu yake aina ya iPhone 14 Pro Max iliibiwa na mtu wa pikipiki na anapanga kufanya kila awezalo ili kurejesha kifaa chake.

Kulingana naye, amefuatilia na kupata eneo ambalo simu hiyo iko akidai iko Mwiki Kasarani Nairobi, Kenya.

“Mwiki sio mbali kwa serikali, tutakukamata kama kuku jua tu siku zako zinahesabika. Katika ujirani wetu, hii haitaendelea lazima uwe mfano." KRG aliandika.

Krg alisema kuwa kuwatafuta au kukimbizana na wezi anapenda sana na ushauri wake kwa mhalifu ni kwamba watoweke na si kumrahisishia kuwapata.

“Kuna Mjinga wa nduthi ameamua leo nitalala mteja. Ushauri wangu kwako ni kukimbia ujifiche kwa sababu nitakupata, na itakuwa mbaya. Ninapenda kuwakimbiza wahalifu ni hobby yangu nyingine. Nitakutoa hadi shimo la maji taka.” Taarifa ya KRG ilisoma