Kanyari adai bado yeye ni “mtumishi wa Mungu” baada ya Pastor T kumuita ‘content creator’

Mchungaji huyo mwenye utata mwingi kwa miaka mingi alisisitiza kwamba licha ya kle kulichotokea katika kanisa lake akikabidhiwa zawadi za kondomu, bado yeye anasalia kuwa mtumishi mtiifu wa Mungu.

Mchungaji wa kanisa la Salvation Healing Ministry, Victor Kanyari amemjibu kwa ukali mwenzake kutoka kanisa la Life Church Limuru, T Mwangi kudai kwamba anachokifanya kwenye mtandao wa TikTok si kuhubiri injili bali kukuza maudhui.

Akirejelea matamshi ya T Mwangi kwamba anachokifanya ni kueneza injili bali uovu, Kanyari alisema kwamba T Mwangi anastahili kuzingatia  mafundisho katika kanisa lake na wala si kufuatilia mahubiri yake.

Mchungaji huyo mwenye utata mwingi kwa miaka mingi alisisitiza kwamba licha ya kle kulichotokea katika kanisa lake akikabidhiwa zawadi za kondomu, bado yeye anasalia kuwa mtumishi mtiifu wa Mungu.

“Pastor T Mwangi anasema eti mimi ni mbaya. Si uniombee. Unasema eti mimi ni mchekeshaji, mimi nikiitwa na Mungu ulikuwa wapi Pastor T? nikiitwa tulikuwa na wewe? Kwa nini unasimama kunitupia lawama? Wewe fundisha Biblia, achana na Kanyari,” Mchungaji huyo alichemka.

Kanyari alizidi kwa kumwambia Pastor T kwamba hakuna siku watafanana, au waumini wao kushiriki katika ibada za mwingine, akisisitiza kwamba yeye bado anasalia kuwa Mtumishi wa Mungu.

“Mimi bado ni Mtumishi wa Mungu. Si lazima tufanane. Hakuna siku watu wako watakuwa washirika wangu, na hakuna siku washirika wangu watakukubali,” Kanyari aiongeza.

Jibu la Kanyari linakuja siku tano tu baada ya Pastor T Mwangi kuelezea sababu zinazomfanya kuhisi Kanyari si mtumishi wa Mungu bali ni content creator kwenye mtandao wa video fupi wa TikTok.

"Anayeitwa mtu wa Mungu kwenye TikTok lazima akomeshwe. Anachofanya hakihusiani na Ukristo, ni uovu mtupu,” alisema.

 “Huyu kwanza huyo si pastor huyo ni content creator ukianglia maadili ya pastor na kile ambayo wachungaji wanafaa kufanya kila ofisi iko na specifications na demand na hakuna demand ame meet ,” alisema na kuongeza kuwa baadhi ya makanisa ni biashara tu sio madhabahu za Mungu.