“Mimi sio therapist!” Vera Sidika amfokea shabiki aliyemuomba kurudiana na Brown Mauzo

Juzi kati, Mauzo alishangaza wengi baada ya kuonekana kudokeza kuchoka na mapenzi, miezi michache baada ya kumtambulisha mpenzi mpya mrithi wa Vera Sidika katika maisha yake.

Muhtasari

• “Baby daddy naumia bila uwepo wako, vitu anavyoviweka kwenye status ni vya kushangaza. Ako depressed, tafadhali rudi tu,” Shabiki huyo alimuomba Sidika.

• “Mimi sio mtaalamu,” Sidika alijibu kwa ukali.

Brown Mauzo na Vera Sidika.
Brown Mauzo na Vera Sidika.
Image: Facebook

Vera Sidika ameonekana kufikwa kooni na matakwa ya baadhi ya mashabiki wake wanaomuomba kila mara kurudiana na baba wa watoto wake, msanii Brown Mauzo.

Hili lilionekana wazi alipomfokea kwa ukali shabiki mmoja ambaye alimuomba kurudiana na Mauzo, kwa kile alidai kwamba msanii huyo kutoka Pwani ya Kenya anaonekana kuteseka kimapenzi tangu walipoachana na mama wa wanawe mwezi Septemba mwaka jana.

Shabiki huyo alimwandikia kwenye DM yake akimuomba kurudiana na Mauzo kwa kusema kwamba anaumia kimapenzi, lakini Vera akamjibu kwa ukali akisema kwamba yeye si mtaalamu wa kushughulikia watu wanaoumia kimapenzi.

Shabiki huyo ambaye anaonekana kuwa mfuatiliaji wa karibu wa shughuli za Mauzo mitandaoni alieleza kwamba ana uhakika juu ya hilo kutokana na jumbe za Mauzo kwenye status zake kuhusu suala la mapenzi.

“Baby daddy naumia bila uwepo wako, vitu anavyoviweka kwenye status ni vya kushangaza. Ako depressed, tafadhali rudi tu,” Shabiki huyo alimuomba Sidika.

“Mimi sio mtaalamu,” Sidika alijibu kwa ukali.

Juzi kati, Mauzo alishangaza wengi baada ya kuonekana kudokeza kuchoka na mapenzi, miezi michache baada ya kumtambulisha mpenzi mpya mrithi wa Vera Sidika katika maisha yake.

“Wanawake watakuja kuniua, nimekwishamalizana nao,” moja ya ujumbe wa kuvuta nyuzi kutoka kwa Mauzo ulisoma.

Wawili hao walithibitisha kuachana mwaka jana kutokana na kile walisema ni kuchokana kimapenzi.

Mpaka kuachana kwao, walikuwa wamechumbiana kwa takribani miaka 3 na kubarikiwa na watoto wawili; wa kike na wa kiume.

Hata hivyo, hivi majuzi katika mahojiano na Kalondu wa Mpasho, Vera Sidika alifichua kwamba anachumbiana na mwanamume raia wa Nigeria lakini akasisitiza kwamba uhusiano wao si rasmi sana kwamba utakomaa hadi kufikia hatua ya kuoana.

Mama huyo wa watoto wawili alisema kwamba kwa sasa hataki kuwa katika uhusiano wa kujiwajibisha kw asana, kwani anazingatia Zaidi uhuru wa maisha yake, kufanya chochote atakacho katika wakati wowote na sehemu yoyote duniani bila vikwazo kutoka kwa mpenzi.