Zuchu amuomba Diamond kufadhili gharama ya kufanyiwa sajari ya maziwa kuwa kubwa

Zuchu alitaka pia kujua kama Diamond atamsubiri hadi apone baada ya mchakato wa kuongeza maziwa au atatafuta mpenzi mwingine wa kukata kiu naye wakati Zuchu anajiuguza.

Muhtasari

• “Utaniuguza ama utatafuta mwingine wa kujishikilia?” Zuchu alimuulzia Diamond tena.

• Wawili hao wamekuwa katika uhusiano wa hali ya vugu vugu, wakiachana na kurudiana mara kwa mara.

Diamond na Zuchu
Diamond na Zuchu
Image: Instagram

Malkia wa WCB Wasafi, Zuchu ameomba mpenzi wake ambaye pia ni bosi wake, Diamond Platnumz kufadhili mchakato wa kuongeza urembo wake kwa kufanyiwa sajari ya kuongeza ukubwa wa maziwa yake.

Katika video ambayo wawili hao walikuwa wanazungumza wakiwa wamekumbatiana kwenye kochi, Zuchu alitoa ombi hilo la mshangao kwa Diamond akimwambia kwamba angependa kufanya sajari ya kuongeza matiti yake na kumuomba Diamond kuwa mfadhili wa mchakato huo.

“Nataka kuenda kufanyiwa sajari ya madodo, nifanye yawe makubwa kidogo, kwa hiyo naweza kwenda? Utagharamia mchakato huo?” Zuchu anaonekana akimuuliza Diamond ambaye kwa dalili zote alikuwa radhi kufanya juhudi ili kuona mpenzi wake anadumisha furaha ya penzi lao.

Katika klipu hiyo, Zuchu pia alimkabili Diamond kwa maswali mengi, akilenga kupata hakikisho iwapo kweli Diaomond anampenda au anamtumia na kumchezea tu kisha kumtema baadae.

Zuchu alitaka pia kujua kama Diamond atamsubiri hadi apone baada ya mchakato wa kuongeza maziwa au atatafuta mpenzi mwingine wa kukata kiu naye wakati Zuchu anajiuguza.

“Utaniuguza ama utatafuta mwingine wa kujishikilia?” Zuchu alimuulzia Diamond tena.

Wawili hao wamekuwa katika uhusiano wa hali ya vugu vugu, wakiachana na kurudiana mara kwa mara.

Hata hivyo, mara ya mwisho walifanya hivyo ilikuja kubainika baadae kwamba walikuwa wanatafuta kiki na baadae kuachia wimbo wao mpya pamoja.