“Niliacha kupoteza nywele baada ya kuiacha ndoa ya mateso” – Mke wa zamani wa Chameleone

Atim aliorodhesha kwamba baadhi ya mambo ambayo yalibadilika katika maisha yake baada ya kuondoka katika ndoa yake ‘ya mateso’ ni pamoja na kuacha kumomonyoka nywele, kuacha kupoteza uzani wa mwili...

Muhtasari

• Daniella Atim, ambaye aliolewa na mwimbaji Jose Chameleone kwa miaka 16, hivi karibuni aliorodhesha mambo 11 ambayo hawezi kumwambia mwanamke katika ndoa yenye unyanyasaji.

Mke wa zamani wa nguli wa muziki kutoka Uganda Jose Chameleone, Daniella Atim ameonekana kuegemea Zaidi katika kutoa ushauri nasaha kuhusu ndoa, katika siku za hivi karibuni tangu kuanzisha chaneli yake ya YouTube, ‘Diary of a retired wife’.

Katika kipindi cha hivi majuzi kwenye chaneli hiyo, Atim alieleza kile alichokitaja kuwa ni mambo 10 ambayo yaliacha kumzonga baada ya kufanya uamuzi wa kuondoka katika ndoa aliyoitaja kuwa ya manyanyaso.

Katika orodha hiyo, Atim aliorodhesha kwamba baadhi ya mambo ambayo yalibadilika katika maisha yake baada ya kuondoka katika ndoa yake ‘ya mateso’ ni pamoja na kuacha kumomonyoka nywele, kuacha kupoteza uzani wa mwili, kuacha kuwa na huzuni miongoni mwa mambo mengine.

Hii hapa orodha kamili kama alivyoielezea;

  1. Huzuni (Macho yangu hayakuweza hata kufungua; nilikuwa nikikodoa kila mara).
  2. Kupunguza uzito (hii haitaji kutajwa).
  3. Kupoteza nywele (Kila mtu alifikiri sina nywele lakini sasa ninakata kila robo mwaka).
  4. Ngozi iliyochoka (Unaweza kusema kwa usalama ‘nali musiwufu’).
  5. Uchovu usioeleweka (Sasa nimefufuliwa na nina nguvu).
  6. Kuvimba kila wakati (Usikumbuke wakati hivi majuzi nilihisi uvimbe).
  7. Kimya na kutengwa (Sikuwa na nguvu… Kwa kweli ninaweza kuzungumza na nimetengwa na ninatoka).
  8. Huzuni
  9. Huzuni
  10. Huzuni

Daniella Atim, ambaye aliolewa na mwimbaji Jose Chameleone kwa miaka 16, hivi karibuni aliorodhesha mambo 11 ambayo hawezi kumwambia mwanamke katika ndoa yenye unyanyasaji.

Tangu kuanzisha chaneli yake ya ‘Diary of a retired wife’ yapata miezi miwili iliyopita, Atim ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani amekuwa akizungumzia mambo mbalimbali haswa kuhusu ndoa, na jinsi alivyokuwa akipitia kile anachokiita mateso kwenye uhusiano wake wa karibia miongo miwili na mwimbaji Chameleone.