“Siwezi rudi Webuye juu mume ame’cheat, nitavumilia tu kwa Mansion Kitsuru” – Risper Faith

"Siku hizi hakuna kuachana, unakwenda wapi baada ya kuachana? Mimi siko tayari kurudi Webuye, nitasalia kwenye jumba la kifahari Kitsuru mpaka mwisho, hata kama atacheat, nitakwama naye,” Risper alisema.

Muhtasari

• Mwanasosholaiti huyo alifichua kwamba alikutana na mpenzi wake katika mtandao wa Instagram kabla ya penzi lao kuota na baadae kuoana.

Risper FAITH.
Risper FAITH.
Image: Instagram

Mwanasosholaiti wa muda mrefu, Risper Faith maarufu kama Lady Risper ameweka wazi msimamo wake kuhusu nadharia ya wanawake kugura ndoa zao pindi wanapogundua kwamba wanaume wao wanachepuka na kuwasaliti kimapenzi.

Akizungumza na Oga Obinna, Risper alisema kwamba yeye hayuko tayari kufuata mkondo huo, kwani nia yake ni kusalia kwenye ndoa yake hadi mwisho wa dahali hata kama mume wake atachepuka kwa kiasi kipi.

Risper alisema kwamba hata siku moja haijawahi muingia akilini kutoroka ndoa yake na kurudi kwao Webuye kwa sababu ya mume wake kuchepuka.

Kulingana naye, atakapogundua mume amechepuka, atamkalisha chini atake kubaini kiini cha kuchepuka ili kumtimizia na kumzuia kutochepuka tena, akisema kwamba yuko radhi kuvumilia ndoa yake na kuishi katika mtaa wa kifahari wa Kitsuru kuliko kufungasha virago na kurudi kwao kijijini, Webuye.

“Nitamuuliza kwa nini alichepuka na kama ilimfurahisha ili pia nifanye maboresho katika kumpakulia kwa mtindo sawia, ni kuelewana. Siku hizi hakuna kuachana, unakwenda wapi baada ya kuachana? Mimi siko tayari kurudi Webuye, nitasalia kwenye jumba la kifahari Kitsuru mpaka mwisho, hata kama atacheat, nitakwama naye,” Risper alisema.

Risper amekuwa kwa ndoa na mumewe Brian Muiriri kwa muda sasa na pamoja wana mtoto mmoja.

Mwanasosholaiti huyo alifichua kwamba alikutana na mpenzi wake katika mtandao wa Instagram kabla ya penzi lao kuota na baadae kuoana.