Crown Media ya Alikiba yaendelea kuzipigia debe nyimbo za wasanii wa WCB Wasafi bila bifu

Hatua ya Crown Media kuweka upinzani baina ya Diamond na Alikiba pembeni na kuamua kupromote kazi zao imepigiwa saluti na wengi ambao pia wanaitaka Wasafi Media kuiga mfano huo

Muhtasari

• Alikiba aliweka wazi kwamba Crown Media litakuwa ni shirika la habari kwa wote na wala si kwa ajili ya maslahi ya family – kama ambavyo Wasafi Media imekuwa ikitajwa kujikita kifamilia Zaidi.

Crown Media, shirika la habari linalohusishwa na umilisi wa msanii wa Kings Music, Alikiba wameendea kuonyesha ukomavu katika kuendesha shughuli zao kwa kuzipigia debe na kuzipaisha nyimbo za wasanii wanaotajwa kuwa ni wa chama pinzani na bosi wao.

Crown FM, kupitia ukurasa wao wa Instagram wamekuwa wakichapisha nyimbo mpya ambazo zimetoka kutoka kwa wasanii mbali mbali na kutoa uchambuzi wa kina kuhusu wasanii husika na takwimu jinsi nyimbo zao zinafanya katika majukwaa mbalimbali ya kidijitali.

Wa hivi majuzi kuingia katika uchambuzi wao ni msanii Zuchu ambaye wimbo wake mpya ‘Siji’ umepata kutambliwa na Crown FM na kushabikiwa kama moja ya nyimbo za hivi majuzi ambazo zinazipi kufanya vizuri kwenye majukwaa ya kidijitali ya kupakua miziki.

Itakumbukwa wiki tatu zilizopita, Crown FM walichapisha wimbo wa Diamond, Komasava kwenye ukurasa wao na kutoa maelezo marefu jinsi msanii huyo ambaye ni bosi wa lebo pinzani a WCB Wasafi lakini pia mkurugenzi katika shirika la habari la Wasafi Media, amefanikisha katika kuleta mageuzi bora kwenye muziki wa Bongo, haswa kwa mtindo wa Amapiano.

Hatua ya Crown Media kuweka upinzani baina ya Diamond na Alikiba pembeni na kuamua kupromote kazi zao imepigiwa saluti na wengi ambao pia wanaitaka Wasafi Media kuiga mfano huo na kuzicheza nyimbo za wasnii wa nje ya lebo yao.

Itakumbukwa mapema mwaka huu wakati wa uzinduzi wa shirika hilo la habari, mkurugenzi Alikiba aliweka wazi kwamba Crown Media litakuwa ni shirika la habari kwa wote na wala si kwa ajili ya maslahi ya family – kama ambavyo Wasafi Media imekuwa ikitajwa kujikita kifamilia Zaidi.

Na kweli, wanaonesha kupitia vitendo na si maneno tu.