logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa nini Pasta Kanyari ametangaza kuacha kuchukua sadaka inayotolewa katika kanisa lake

Kuanzia leo sadaka zangu zote zitaenda kuwasaidia wasiojiweza - Kanyari.

image
na Davis Ojiambo

Burudani31 May 2024 - 10:29

Muhtasari


  • • Mchungaji huyo alionekana akipokezwa zawadi za kondomu na vitu vingine vya mapenzi, jambo ambalo lilizua joto jingi kutoka kwa Wakenya ambao walimzomea vikali.

Mchungaji mwenye utata kutoka kanisa la Salvation Healing Ministry, Victor Kanyari ametangaza kuacha kuchukua sadaka zinazotoewa katika kanisa lake kuanzia sasa kwenda mbele.

Mchungaji huyo ambaye haishi visanga na vimbwanga haswa kwenye mtandao wa video fupi wa TikTok alitangaza taarifa hizi kupitia mtandao huo, akionesha kuchukua mkondo tofauti.

Licha ya wengi kumtaja kama mchungaji mpenda pesa, Kanyari ameonekana kuchukua mkondo kinyume na dhana hiyo ambapo ametangaza kwamba hatakuwa na haja na sadaka za watu, kwani zitakazotolewa hazitaenda katika mifuko yake bali katika kuwasaidia wasiojiweza kwenye jamii.

“Nimeamua kuanzia leo sitakuwa nachukua sadaka. Kuanzia leo sadaka zangu zote zitaenda kuwasaidia wasiojiweza. Kwa hivyo, kanisani kila Jumapili tutakuwa tunawasaidia wasiojiweza,” Kanyari aliweka malengo yake wazi.

Mchungaji huyo ametangaza haya siku chache baada ya kuzua joto la minong’ono mitandaoni baada ya kupokea zawadi za ajabu kutoka kwa mrembo tiktoker katika kanisa lake kama dhabiu.

Mchungaji huyo alionekana akipokezwa zawadi za kondomu na vitu vingine vya mapenzi, jambo ambalo lilizua joto jingi kutoka kwa Wakenya ambao walimzomea vikali.

Hata hivyo, Kanyari alinywea kutokana na presha hizo na kulazimika kuomba radhi akisema kwamba hilo halitajirudia tena katika kanisa lake, huku akisema kwamba aliteleza kutokana na kuwa mwanadamu kama wengine tu.

Kanyari alijiunga TikTok miezi michache iliyopita na kuwasuta waliomsimanga kuwa alifuata pesa akisema kuwa kilichompeleka TikTok ni kuwahubiria vijana wanaozingirwa na ibilisi katika mtandao huo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved