Amber Ray atoa masharti magumu kwa yeyote anayetaka kuwa rafiki yake

"Kama huna kitu chochote, kwa nini sisi ni marafiki? mimi ni mtoaji," alisema.

Muhtasari

• Mimi ni mtoaji, na nimejifunza kwa njia ngumu. Inakuwa rahisi wakati kila mtu ana utulivu wa kifedha kwa sababu tunapaswa kupanga hata sherehe yetu," alisema.

•Alisisitiza kwamba asingemchukua mtu yeyote ambaye hatakuwa akiongeza thamani ya maisha yake.

Amber Ray
Image: HISANI

Mwanasosholaiti mashuhuri wa Kenya Faith Makau almaarufu Amber Ray ametoa masharti maalum ambayo mtu anahitajika kutimiza ili kuwa rafiki yake.

Akizungumza wakati wa hafla kubwa ya ufunguzi wa duka la nywele na urembo la rafiki yake Phiona, Amber Ray alisema ili mtu awe rafiki yake, anatakiwa kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kifedha ili waweze kusaidiana.

“Saa hizi vile maisha imekuwa kwa mimi kuwa rafiki na wewe, nataka uwe stable. Juu nikiwa na shida na wewe uko na shida tusaidiana aje sasa.” Amber Ray alisema.

Mama huyo wa watoto wawili alisema anapendelea iwe hivyo kwa sababu alijifunza kwa njia ngumu na sasa ameamua kuchukua watu ambao wanaongeza thamani ya maisha yake.

"Kama huna kitu chochote, kwa nini sisi ni marafiki? mimi ni mtoaji, na nimejifunza kwa njia ngumu. Inakuwa rahisi wakati kila mtu ana utulivu wa kifedha kwa sababu tunapaswa kupanga hata sherehe yetu. Amber aliongezea.

Alisisitiza kwamba asingemchukua rafiki yeyote ambaye hatakuwa akiongeza thamani ya maisha yake kwa sababu watakuwa wanamrudisha hivyo kufanya iwe vigumu kwake kujisimamia mwenyewe na kufanya chochote.