Hisia mseto baada ya Bahati na Diana Marua kuvaa nguo za kike zinazofanana (+video)

Sababu ya Kukaa nyumbani katika Likizo hii ya Madaraka Day #TheBahatis

Muhtasari

β€’Bahati alichapisha video akiwa amevalia vazi jekundu lililolingana na mkewe, Diana Marua, jambo lililowafurahisha na kuwaudhi wengi mtaondaoni.

β€’Sehemu ya wanamtandao walimkashifu mwanamuziki huyo aliyegeuka-mwanasiasa kwa kufaa nguo za bibi yake.

DIANA MARUA and BAHATI
Image: INSTAGRAM//

Mwanamuziki Kelvin Kioko almaarufu Bahati kwa mara nyingine tena amezua hisia mseto baada ya kuvalia nguo sawa na bibi yake Diana Marua.

Baba huyo wa watoto watano alishiriki video akiwa amevalia mavazi mekundu yanayolingana na mkewe, Diana Marua, mnamo Juni 1, Siku ya Madaraka.

Wapenzi hao pia walilinganisha mikoba na viatu virefu, na kuwaacha mashabiki wao wakiwa wamefurahishwa.

Bahati alisema kuwa sababu ya kutotoka nje ni kwa sababu waligundua walikuwa wamevalia mavazi yanayolingana.

"Sababu ya Kukaa nyumbani katika Likizo hii ya Madaraka Day #TheBahatis,” aliandika.

 

Wakijibu video hiyo, baadhi ya mashabiki walimkashifu mwanamziki huyu kwa tukio hio

Miss.shakes said:

 "Y'all my favourite couple right there ❀️❀️."

Vancekims said:

 "Our incoming MP for Mathare."

Billwonderke said:

 "It is not funny anymore."

 Warsameresofficial said:

Your favourite MP ‍♂️."

 Davinchiclassic said:

 "This is becoming too much buana."

Evline_madowo said:

 "Have just realized that Bahati is more curvier than me ."

 Its_ajaab said:

"This is the guy who was crying for his mom's love and now this."

 Namelesskenya said:

 " I knew it."